






***************
Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) kimeshiriki maonyesho ya Vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Juu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Maonyesho hayo ya siku Saba yameanza tarehe 07 - 13/06/2022 yamejumuisha Vyuo mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt. Lucas Mwisila ametoa wito kwa umma wa Tanzania kujiunga na Chuo hicho kutokana na fursa zilizopo katika tasnia ya bahari.
Dkt. Mwisila amesema Kwa sasa dirisha la udahili lipo wazi kwa ngazi ya Cheti na Diploma, hivyo anawakaribisha watanzania na wasio watanzania kujiunga na chuo cha bahari Dar es Salaam.
Chuo cha bahari dar es Salaam kinatoa kozi za ubaharia zikiwemo Uendeshaji wa meli (Unahodha), Uhandisi wa meli, Usimamizi wa masuala usafirishaji na lojistiki, Uhandisi wa mafuta na gesi na nyingine nyingi ambazo zinatolewa Kwa ngazi ya Cheti, diploma, digrii na Uzamili.
Aidha chuo kinatoa kozi fupi pamoja na kozi za umahiri kuhusiana na tasnia ya bahari.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kozi zitolewazo na chuo cha DMI unaweza kutembele tovuti ya chuo www.dmi.ac.tz au unaweza kupiga simu 0688 941 921/ 0716 898 037
Post A Comment: