Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na michezo.Mhe, Mohamed Mchengerwa ameitaka Timu ya
soka ya walemavu ya (Tembo Warriors) kutumia mechi za maandalizi na
nchi mbalimbali za Ulaya kujinoa ili kushinda kombe hilo na kulirejesha
nchini.
Mhe
Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2022 uwanja wa Benjamini Mkapa
wakati akiikabidhi bendera ya Taifa timu hiyo akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi inayokwenda kuanza kucheza mashindano
kwenye maandalizi na timu mbalimbali za Ulaya kwa kuanzia na timu ya
Poland ili kuweza kupata uzoefu wa kucheza na nchi za mabara mbalimbali
kabla ya kuanza mashindano haya.
“Tumeamua
kama Serikali kuendelea kuhaakikisha kuwa tunazisaidia timu zinazofanya
vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ili kuwasaidia kukuza ajira na
kuwafanya waajiriwe kwenye vilabu vikubwa duniani” amefafanua Mhe.
Mchengerwa
Amesema
watanzania wamechoka kuona kuwa nchi inasuasua kwenye michezo na
amesisitiza kuwa wakati huu watanzania wanataka kombe la dunia kuja
Tanzania ambapo amesema hilo litafanikiwa kwa kuweka mbele utaifa na
uzalendo wanapokuwa kwenye mashindano haya.
Ameongeza
kuwa jambo kubwa kwa sasa ni kuwa na nidhamu na kuzingatia misingi
ambayo wanapewa na makocha wa timu zao ili waweze kufika mbali na
kuboresha maisha yao na uchumi wan chi yetu kwa ujumla.
“Naomba
kuwaambia mkifanya vizuri katika mashindano haya ya maandalizi tu nina
uhakika mtanunuliwa na timu kubwa na mtabaki ulaya, mtabadilisha
maisha ya familia zenu na watanzania kwa ujumla” ameongeza Mhe.
Mchengerwa
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti viongozi wa timu hiyo wamemwahidi Rais wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania kuwa wanakwenda kuanza kutema cheche katika
maandalizi ya timu hizo za awali ili kujihakikishia kutwa kombe hilo.
Katibu
Mkuu. Dkt, Abbasi amesema Tembo Warriors ndiyo timu ya kwanza nchini
kufuzu kuingia kwenye mashindano hayo na kuitaka kuendelea kushikilia
heshima hiyo kwa kuwa timu ya kwanza kurejesha kombe nyumbani.
Post A Comment: