KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani
kuhusiana na tuzo walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban katikati akiwa amebeba Kombe la Ushindi na tuzo ikiwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Banda lao mara baada ya kukabidhiwa
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban katikati akiwa amebeba Kombe la Ushindi na tuzo ikiwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Banda lao mara baada ya kukabidhiwa
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
KAIMU
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga
(Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban amesema mamlaka hiyo imetumia zaidi
ya Shs Milioni 150 kwa ajili ya kuagiza mita za malipo ya kabla
(pre-paid)toka Nchini Ufaransa.
Mhandisi Shabani aliyasema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo
walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa.
Mhandisi
Shabani alisema kumekuwepo na malalamiko kwa wateja yanayohusu madai ya
kuongezewa gharama za malipo(bili) ambapo mita hizo ndio zitakuwa
muarobaini wa malalamiko hayo.
Aidha alisema Mamlaka hiyo
imefanya tafiti za kutosha na kubaini kwamba wananchi wengi hawajatambua
tatizo la ongezeko la bili ya maji hivyo kuanza kutafuta mbinu mbadala
ya kumaliza tatizo hilo.
Alisema lengo ni kukidhi hitaji la
Serikali la kutaka wananchi waweze kupata huduma ya maji katika maeneo
yote kwa Mijini na Vijijini.
“Tumeanza kufanya tathmini kama
tulivyoagizwa na Wizara kuhusiana na mita hizi za malipo ya
kabla(pre-paid) na tathmini yetu iko vizuri na matarajio yetu
tutafanikiwa”Alisema Mhandisi Shaaban.
Alisema matarajio kuanza
na mita 500 ambapo Mamlaka hiyo imepanga kuzifunga kwa baadhi ya wateja
kama sehemu ya majaribio na mafanikio yake ndio yatakayopelekea kufungwa
kwa mita hizo Mkoa Mzima.
“tumeshaanza majaribio ya mita hizo
na zinaonekana kuwa na tija lengo letu sasa ni kuhakikisha tunazisambaza
Mkoani kote ”Alisema Mhandisi Shaaban.
Mhandisi Shabani
alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi Mkoani Tanga kupokea huduma hiyo
na watakuwa na uwezo wa kununua maji kutokana na uwezo wa mteja kama
inavyofanyika katika huduma nyingine za kijamii.
Hata hivyo
alisema Mamlaka hiyo imepokea tuzo ya watoa huduma bora dhidi ya Mamlaka
za Serikali zilizokuwepo kwenye maonyesho hayo kwa kupatiwa cheti na
ngao na ile ya ushindi wa Jumla.
Mwisho
Post A Comment: