Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kuchukua Hatua za kisheria dhidi ya Watumishi waliofanya ubadhirifu wa fedha za mapato ya Halmashauri.
Mongela ameyasema hayo leo alipohudhuria katika kikao maalum cha kujibu hoja za Mkaguzi wa mahesabu ya Serikali CAG kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Karatu nakueleza kuwa halmashauri inatakiwa kuboresha njia ya ukusanyaji wa mapato ili kuepeusha kupotea Kwa mapato ya Serikali.
Aidha Rc Mongela ameigiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) sambamba na Jeshi la Polisi kufanya upelelzi juu ya wazabuni wote waliopewa dhamana ya kukusanya mapato ambao wamefanya ubadhirifu wa fedha hizo na kufikishwa mahakamani
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Dkt. John Lucian Mahu amesema Baraza la madiwani halitakubali kuwavumilia Watumishi wazembe na wezi ambao wanaohujumu fedha za serikali.
Sambamba na Hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia suluhu Hassan Kwa kuongeza fedha za miradi katika Halmashauri hiyo iliyotekelezwa katika Hospital ya Wilaya,ukarabati wa Shule ya sekondari ya Karatu,Nyumba za Watumishi, sambamba na ujenzi wa Shule mpya iliyogharimu zaidi ya millioni 400.
Post A Comment: