Na,Jusline Marco;Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira Halmashauri ya Meru, Lucas Kaaya amewataka wakazi wa Arumeru kutii sheria za mazingira kutoharibu ekolojia kwa kutojenga katika hifadhi za vyanzo vya maji.
Lucas ametoa kauli hiyo katika kilele cha Siku ya Mazingira ambapo amesema utupaji wa taka hovyo zinazohatarisha ekolojia na kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji kunakatazwa na sheria za usimamizi wa mazingira na afya ya jamii.
Aidha amewataka wananchi hao kuheshimu elimu wanayopewa na wataalam wa serikali na wadau mbalimbali wa masuala ya mazingira na kuwaagiza kuona utunzaji wa mazingira kuwa ni jukumu lao kwa kufufua na kulinda ekolojia kwa maendeleo endelevu.
Aidha amesema Halmashauri ya Meru imekabiliwa na changamoto hatarishi ikiwemo kutokuwa na miundombinu madhubuti ya kuhifadhi taka ngumu na laini pamoja na uharibifu wa mazingira na mifumo ekolojia kutokana na uchimbaji haramu wa mawe maeneo yasiyoruhusiwa.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Halmashauri ya Meru Charles Mboya amesema kama halmashauri wanakusudia kupanda miti milioni 1.5 ifikapo juni 31 mwaka huu ili kufikia lengo la taifa kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa kuvamiwa na wananchi kwa kufanya shughuli za kilimo na makazi katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 pamoja na mabadiliko ya tabianchi ni moja kati ya vyanzo visabanishi vya uharibifu wa mazingira.
Amesema kuwa madhumuni ya maadhimisho hayo ni kuelimisha na kuhamasisha jamii kuwa mstari wa mbele katika kuchukuwa hatua za kuhifadhi mazingira,kutoa fursa kwa wananchi kutambua wajibu wao na kuelimisha jamii juu ya matumizi endelevu ya mazingira.
Naye Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Ndg.Lewis Nzali amesama mazingira yamekuwa yakichafuliwa na utupaji holela wa takataka ambapo ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa ya mazingira katika kutenganisha taka ili kuweza kuyaweka mazingira safi na kulknda vyanzo vya maji.
"Katika usimamizi wa taka za majumbani ni vyema kila mtu nyumbani kwake ajenge utamaduni wa kutenganisha taka kwa kuweka vyombo zaidi ya kimoja ambapo kimoja anaweza akaweka mabaki ya vyakula anbayo yanaweza kutumika kutengeneza mbolea kwa ajilj ya bustani nyumbani."alisema Nzali
Vilevile Nzali ameongeza kuwa kwa taka nyingine kama taka ngumu na kusema kuwa taka hizo zinaweza kurejelezwa kwa kutengeneza vitu vingine kama milango,Viti na meza ambapo anesema faida ya kutenga taka hizo ni urasishaji na urejeleshaji.
Post A Comment: