Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Kampuni ya REO Communications kutoka Hongkong inayojishughulisha na utangazaji wa maeneo ya uwekezaji ya nchi mbalimbali barani Afrika kwa njia ya majarida.


Kikao hicho kimefanyika leo Juni 29, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.


Mhe. Masanja amewapongeza watendaji hao kwa nia nzuri ya kutaka kutangaza maeneo ya uwekezaji pamoja na vivutio vya utalii vya Tanzania.


Aidha , ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafanikiwa katika adhima hiyo.


Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya REO Communications nchini Tanzania, Xhovana Kelmendi alisema lengo ni kuhakikisha wanatangaza maeneo ya uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo Utalii, Kilimo, Madini n.k.


Amesema wameshafanikiwa kutangaza maeneo ya uwekezaji katika nchi ya Indonesia na wana miradi ya aina hiyo ambayo inaendelea katika nchi za Kuwait, Morocco, Nigeria, Malta na Tokyo.


Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya kukutana na wadau wa Sekta ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka.

Share To:

Post A Comment: