Na Mwandishi Wetu.

Kituo cha Kulelea Watoto Yatima (Msongola Orphanage Trust Fund) kilichopo Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala kinakabiliwa na Uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watoto kituoni hapo.

Changamoto hiyo imeelezwa na Mlezi wa Kituo hicho Bi. Christina Haule kwa  Mwanaharakati Huru Bwana Bihimba Nassoro alipotembelea kituo hicho  kutoa msaada wa viatu na nguo kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.

Aidha Bwana Bihimba ameahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kupunguza ukubwa wa changamoto hiyo na kutoa rai kwa yeyote mwenye kuguswa na jambo hilo kujitolea kuwasaidia watoto hao ili waweza kupata chakula cha kukidhi mahitaji yao.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: