Na;Jusline Marco;Arusha
Halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru inatarajia kupokea mwenge wa Uhuru 2022 mnamo tarehe 23.06.2022 majira ya saa 12.00 asubuhi katika viwanjwa vya shule ya Sekondari Oldadai kata ya Sokon II, ukitokea halmasahuri ya Jiji la Arusha.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Suleiman Msumi amesema mwenge huo utakimbizwa Kilomita 90.4 na kutembelea jumla ya Miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 katika sekta Elimu, Afya, Maji, miundombinu ya Barabara pamoja na uwekezaji wa viwanda.
Aidha amewataka wananchi wote kujitokeze kupokea na kuukimbiza mwenge huo wenye kailo mbiu ya SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO, SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA".
Post A Comment: