Naibu kamishna wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt Christopher Timbuka akizungumza kwenye kikao Maalimu na Waandishi wa Habari kilichofanyika jijini Arusha leo Juni 29, 2022,akieleza kuhusu taarifa zilizoripotiwa hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna Ng’ombe wamekufa baada ya kuhamia Kijiji cha Msomera ambazo hazina ukweli na kueleza kuwa picha hizo ni za Ng’ombe waliokufa katika nchi ya Jirani kutokana na matatizo ya ukame mwaka 2018.
NAIBU Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dk.Christopher Timbuka amefafanua kwa kina kuhusu mazoezi yanayoendelea katika hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Loliondo huku akitumia nafasi hiyo kukemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wanaotaka kuhamishwa katika mchakato huo.
Akizungumza leo Juni 29,202 mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Maurus Msuha, Naibu Kamishana wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro amesema amefurahi kutolewa kwa wasilisho lenye lengo la kutoa uelewa wa pamoja na sahihi kuhusu mazoezi yanayoendelea katika maeneo ya Loliondo na Ngorongoro
“Lengo la kufanyika kwa wasilisho hili ni kuondoa mchanganyiko unaowekwa katika jamii yetu na jamii ya kimataifa kwa makusudi au kwa kutokufahamu.Tunashukuru tumepata ufafanuzi wa hoja zilizopo mbele yetu, kuna hoja ya Ngorongoro na hoja ya Loliondo na hizi zote zinajitegemea.
“Kinachofanyika huko ni kama kilivyowasilishwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori na lengo ni kupata uelewa wa pamoja kama tulivyofanya kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kwetu.Uelewa ambao wamepatiwa wawakilishi hao ndio huu huu ambao unatolewa kwetu maana meseji ni moja.
“Na hii itatusaidia kuondoa upotoshaji kama tulivyoona kwenye mitandao ya kijamii ,kumekuwa na kuchafua mazoezi haya kwa makusudi, watu wanaweka stori ambazo sio sahihi, kwa mfano picha zinazozunguka kwenye mitandao ikionesha mifugo iliyohamishwa kutoka Ngorongoro imekufa kutokana na ukame wakati sio kweli.
“Hali halisi picha hizo ni za mwaka 2014 na 2016 ambazo zilipigwa nchini Kenya wakati huo kwenye nchi hiyo ulipita ukame mkali uliosababisha watu kupoteza mifugo yao.Hivyo wanaosambaza picha hizo hivi sasa lengo lao halijukani,”amesema.
Ameongeza hivyo haiwezekani wazalendo wa nchi yetu kukaa kimya wakati upotoshaji ukiendelea.“Sasa sisi wazelendo wa nchi hii tunategemewa sana kufikisha ujumbe kwani wengine wamepanga kufanya upotoshaji kwamba jambo linalofanywa linakiuka haki za binadamu lakini ninyi nyote mmeona shuhuda kutoka kwa wale waliohamia Msomera na wote wanafurahia sana maisha. Hata yule aliyekuwa tajiri mkubwa sana Ngorongoro Foibe naye anafurahia sana huku.”
Kuhusu zoezi la Loliondo amesema watu hawahamishwi ila kuna upotoshwaji unafanywa, kwa hiyo wameona ni vema ukatolewa ufafanuzi wa masuala yote hayo ili jamii iweze kufahamu.“Suala la elimu na usimamizi limefanyika sana , zoezi la kuweka mipaka kwenye pori tengefu la Loliondo lilianza tangu mwaka 1951 na limekuwa likifanyika sana.
“Na katika miaka 32 kumekuwa na majadiliano kwamba kifanyike hiki , kifanyike kile lakini watu wenye nia ovu wamekuwa mara nyingi wakilipindisha zoezi hili au kutumia mbinu mbalimbali baada ya muda fulani zoezi lisimame.Serikali imeelewa na imelifanya kwa umakini na sasa eneo hilo watalilinda .
“Kama wangesimamisha tena zoezi hilo mwaka huu basi hekari 1500 zingetoweka kwa hiyo ilikuwa lazima hatua zichukuliwe ili kulinda hifadhi zetu na hilo ndio ilikuwa lengo kubwa na limefanikiwa.Kikubwa watu wawe na uzalendo, na watu sio kwamba hawafamu, bali wanafahamu sana , kuna watu wengine taarifa zao zinakuwa sio sahihi kwasababu wanazipokea kwenye vyanzo ambavyo sio sahihi .
“Kwa mfano kuna mtandao mmoja wanasayansi wameandika wakizungumzia masuala ya Loliondo na Ngorongoro , hakuna chembe ya ukweli , hakuna uthibitisho lakini ameandika utadhani alikuwepo na amekuwa sehemu ya hiyo habari,”amesema.
Aidha amesema katika kuondoka kwa hiyari kwenye hayo maeneo ya Ngorongoro sio Wamasai tu ndio waliohama kwa hiyari, bali kuna makabila zaidi ya matatu.Pia kuna wafanyakazi na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni sehemu ya watu waliohama kutoka kwenye eneo la hifadhi kwenda nje na wametumia gharama kubwa.
“Wamejenga majengo makubwa ya ofisi maeneo ya Karatu ambayo yamewagharimu sana na katika kuhama inahusisha pia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, hoteli zote wameziacha na wafanyakazi ambao wanakuwa hawako zamu watakuwa wanakaa nje.Kwa hiyo wanaohamishwa sio kabila moja bali ni wote pamoja na wahifadhi.
“Kuna watu wanazunguzia suala la usanii kwa maana ya wanaohamishwa ni wale watu wa kuja ambapo inawezekana ikawa hivyo lakini kuna uchambuzi wa kina umefanyika ambapo mnaweza kuona hata viongozi wanaohama pale ni wenyeji , ni wachache wanaweza kutokea kwa mfano eneo kama la Kimba.
“Ambapo kulikuwa na wafanyabiashara wengi kwa hiyo kivyovyote utakuta watu wengine sio wenyeji kwa uasili wa maeneo hayo lakini wao wanaowandoa ni wakazi wanaoishi maeneo ya Ngorongoro, kwa hiyo kuna wachache wanaweza kuwa sio wenyeji lakini wameishi pale kwa muda mrefu,”amesema.
Kuhusu suala la kumuuzia mtu mwingine vifaa vilivyobakia baada ya wengine kuondoka amesema wataendelea kulisimamia ili ujenzi usifanyike ikiwa ni hatua ya kudhibiti ujenzi wa holela na kwamba wameongeza nguvu kwa maana mtu akianza kujenga tu anamfuata na kuuliza inakuaje kwani ili ujenge lazima uwe na kibali.
Post A Comment: