![]() |
![]() |
Na John Mapepele,
Kiongozi
Mkuu wa madhehebu ya Kiislamu ya Mabohora (Dawoodi Bohoras); Sheikh
Syedna Mufaddal Saifuddin, ametua nchini leo Alhamisi Juni 16, 2022,
tayari kufanya ziara ya kiimani na mapumziko mafupi.
Saydna
Mufaddal, atakuwa nchini kwa takribani wiki mbili ambapo pamoja na
shughuli za kiimani amekuja kuunga mkono azma ya Rais Samia Suluhu
Hassan ya kuitangaza na kuifungua nchi hasa kupitia filamu ya Royal
Tour.
“Akiwa nchini
amekuja kuunga mkono malengo ya Royal Tour na yeye mwenyewe na wafuasi
wake watakwenda mapumziko hapa nchini na msafara wake wote katika maeneo
mbalimbali na pia iwapo taratibu zitakamilika na akaridhia anaweza
kufanya mhadhara wake mkubwa wa kidini Julai hapa nchini ambapo wafuasi
wake kati ya 30,000 hadi 40,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani
humfuata na tunajipanga ikitokea hivyo tutawaonesha watu hao na mabohora
wengine duniani filamu ya Royal Tour,” alisema mmoja wa viongozi wa
dhehebu hilo nchini Bw. Zainuldeen Adamjee.
Akimpokea
Kiongozi huyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed
Mchengerwa amesema amewasilisha kwa kiongozi huyo salaam za Mhe Rais
Samia ikiwemo utayari wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mhadhara mkubwa wa
mwaka wa kiongozi huyo utakaoleta maelfu ya watu hapa nchini.
“Hii
ni sehemu ya muendelezo wa Royal Tour (post royal tour) ambapo Mhe Rais
wetu amefanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi yetu na sasa wawekezaji na
watalii wakiwemo viongozi wa kimataifa wa kiimani na wa kijamii nao
wanazidi kuja Tanzania. Kwa eneo letu sisi la utamaduni tumemhakikishia
Sheikh kuwa Tanzania ni salama na aendelee kutuombea amani lakini pia
alete wafuasi wake wengi zaidi kuja kutembelea na kuwekeza Tanzania,”
alisema Waziri Mchengerwa.
Katika
mapokezi hayo, Waziri Mchengerwa, aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia anasimamia Kamati ya Rais
iliyoratibu Royal Tour.
Post A Comment: