Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wazazi,wanafunzi na wadau wa shule ya sekondari ya Nyang'oro namna ya kutatua chngamoto ambazo shule hiyo inazikabili.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshika bango ambalo linaonyesha kufikisha kwa miaka kumi kwa shule hiyo
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameinua mkono wa heshima mara baada ya kuzalishwa sskafu na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa maazimisho ya miaka kumi ya shule hiyo
Baaadhi ya wadau na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi ambaye Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya Nyang'oro wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi ambaye Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WANANCHI na wadau wameiomba
serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutatua changamoto ya maji katika
shule ya sekondari ya Nyang’oro iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa ili
kuwasaidia wanafunzi kusoma bila kuwa na usumbufu wa kutafuta maji muda wa
masomo.
Akizungumza wakati wa miaka kumi
ya kuanzishwa kwa shule ya Nyang’oro Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela alisema kuwa shule hiyo toka ianzishwe haijawahi kupata huduma ya maji
hivyo amemuomba Waziri wa maji Juma Aweso kuwafikiria shule hiyo hata
kuwajengea kisima cha maji ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao.
Kasesela alisema kuwa anatambua juhudi
kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wananchi na taasisi mbalimbali
zinapata maji kadili inavyowezekana hivyo anaimani na serikali ya awamu ya sita
kuwa watasikia kilio cha wanafunzi wa shule ya Nyang’oro kutatua changamoto ya
maji ambayo wanakabiliana nayo.
Alisema kuwa anaipongeza Serikali
kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakaa sehemu salama na
hivyo kuwafanya wasome kwa bidii huku akilishukuru shirika la Lyra In Africa
kwa ujenzi wa bweni la wasichana lililochukua zaidi yawanafunzi wa kike 100.
Kasesela aliwataka wanafunzi kuongeza
maarifa wawapo shuleni ili hata wakimaliza waweze kuwa na uwezo wa kujiajiri
kuanzia elimu ya kidato cha nne na kuacha tabia ya kusoma huku wakitegemea
kuajiliwa jambo ambalo linapelekea vijana wengi kukosa ajira pindi wamalizapo
masomo yaona wawe mfano wa kuleta mabadiliko katika jamii
“Wanafunzi upo umuhimu wa kusoma
ukipata daraja la nne ukipata zero sio mwisho wa maisha lakini utakuwa umekwama
utakuwa umepoteza miaka mnne yote maana ya elimu cha kwanza maisha kinakujengea
uelewa kinakuongezea uthubutu sasa kuna wazazi wengine hawataki kupeleka watoto
shule hawajui wanawashushia uthubutu unaweza kuwa billionea lakini ukaliwa hela
na watu wengine ” alisema Kasesela
Kasesela alimpongeza Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ujenzi wa shule za
serikali pamoja na kuongezeka kwa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za uviko 19
na alisema kuwa anawapongeza kutokana na juhudi walizozifanya katika kuboresha miundombinu
ya shule pamoja na kuongeza madarasa kwani wamesaidia wanafunzi waliowengi
kuondokana na adha ya kusomea nje .
“Hatuwezi
kukaa kimya bila kumshukuru Dkt. Kikwete kwa kuanzisha hizi shule alipotoa hili
wazo kulikuwa na upinzani wa hali ya juu watoto nyinyi hamjui kulikuwa na shida
sana zikaanzishwa shule za kata zikasurvive ilikuwa ikifika disemba alafu uko
chini ya magufuli ulikuwa hulali lakini jembe limekuja Mama Samia Suluhu Hassan
ametuondolea adha hii huyu mwana mama maana ya kuupiga mwingi watu hawafahamu
tulikuwa na fedha za uviko yeye kwa ajili ya matibabu yeye akapeleka proposal
tofauti kwamba pamoja na matibabu kuna haya ya madarasa ” alisema Kasesela
Katika hatua nyingine Kasesela
alitoa wito kwa Watendaji kuhamashisha shule nyingine kufanya maadhimisho ili
kuendelea kutambua mchango wa shule pamoja na kufurahi kwa pamoja huku
ikiwatumia hata wahitimu waliomaliza miaka iliyopita kutoa hamasa kwa wanafunzi
wenzao
“Mwakilishi kama yupo
azihamasishe shule nyingine kukutana kusheherekea miaka 10,20,25,50 kuhakikisha
mnaelezea mema yaliyofanyika nawapongeza kwa kufanya hili na kuunda mradi huu
mradi huu mimi nasema umekamilika wala usihofu ” alisema kasesela
Kwa upande Mkuu wa shule ya
sekondari ya Nyang’oro Mwl.Lambert Mdeke alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na wanalishukurushirika la LYRA IN
AFRICA,CAMFED tanzania ,NMB tawi la ruaha na compation tanzania kwa msaada
wanaoendelea kuutoa shuleni hapo kwa wanafunzi wasio na uwezo kiuchumi
“Baadhi ya wafadhili ni LYRA IN
AFRICA waliojenga hostel ya wasichana na kuwafadhili chakula wanafunzi kumi
kila mwaka na pia kutufungia compyuta 11 na kupata material kutoka katika
kompyuta hizo shirika linguine ni CAMFED linalowafadhili wasichana 12 na
kuwapatia mahitaji muhimu kila mwaka na madati 30 ,aidha nmb tawi la ruaha
pamoja na shirika la COMPATION TANZANIA kwa kuwafadhili ada ya hostel wanafunzi
wa kike 22 kanisa la kkkt kihorogota”
Alisema kuwa shule inampango wa
kuanzisha kitege uchumi cha shule mradi utakaosaidia kuongeza kipato cha shule
pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanafunzi na watu waliopo
mazingira ya shule
“Tunataka kuwa na kitega uchumi
cha shule kupitia elimu ya kujitegemea mradi huu utasaidia kutoa huduma za
kijamii kwa wanafunzi nawaliopo mazingira ya shule tutakuwa na duka la mahitaji
muhimu ya binadamu,duka la mahitaji ya kitaaluma ,huduma nyingine chumba cha
mahitajhi ya chakula inafahamika kama restaurant”
David Ngonyani ni Mwenyekiti wa
Bodi ya shule ya Nyang’oro alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa huduma nzuri
inayotolewa shuleni hapo bado kuna changamoto ya baadhi ya wazazi kushindwa
kuwapeleka wanafunzi waliofaulu shule ya msingi na hivyo kushindwa kupata elimu
kama inayotakiwa
Alisema kuwa wazazi wanapaswa
kutoa michango kwa ajili ya chakula kwani wazazi wamekuwa wakizembea kutoa
mahitaji kwa watoto wao na kupelekea baadhi yao kuwa watoro na kuwa na ufaulu
usioridhisha
Naye mwakilishi wa shule ya
sekondari Isimani Mwl.Christopher Mwasomola ameipongeza shule ya sekondari
nyang’oro kwa kutoa wanafunzi wenye vipaji na ujuzi wa kutosha na hivyo kuomba
ushirikiano kuendelea kutolewa ili kukuza kizazi chenye tija .
“pale isimani tunapokea watoto
wengi wanaotoka nyang’oro sekondari hawajawahi kutuiangusha kwa maana hiyo
mnawaandaa watoto vizuri kuna mtoto pale ametoka pale alitoka huku ameandika
riwaya amemaliza kwa hiyo haya maandalizi alitoka nayo na yupo chuo saizi huku
akaja pale tukamuongezea nawapongeza sana pamoja na mazingira magumu lakini sio
kwenye kazi zao”
katika maadhimisho hayo aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alifanikiwa kukusanya fedha za harembee zaidi ya Shilingi Millioni sita fedha ambayo itasaidia katika ujenzi wa karantini ya shule itakayosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii shuleni hapo Shule ya Sekondari Nyang’oro imefanikiwa kutoa huduma ya elimu kwa wanafunzi 631 ambapo wasichana 385 wavulana 246 pamoja na kuwa na bweni la wasichana lenye zaidi ya wanafunzi 100 .
Post A Comment: