Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Sophia Kizigo akiwaonesha Wananchi wa Kata ya Iguguno korosho ambazo kwa mara ya kwanza zimeanza kuzalishwa wilayani humo wakati wa mkutano wa kupokea kero ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge uliofanyika jana.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Sophia Kizigo akifurahi waakti akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge baada ya kumkabidhi korosho ambazo kwa mara ya kwanza zimeanza kuzalishwa wilayani humo wakati wa mkutano wa kupokea kero za wananchi uliofanyika jana Kata ya Iguguno.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge. akizungumza na wananchi wa Kata ya Iguguno wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama wakiserebuka wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi pamoja na mapokezi ya Mwenge Uhuru ambao utalala katika kata hiyo mara utakapo wasili wilayani humo, uliotungwa na vijana wa kata hiyo na ndani yake kuchombwezwa maneno na DC Kizigo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Lucas Mwakatundu akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Singida, Agustino Mwakyembe akizungumza kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa kwenye mkutano huo.
Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Phaustine Ngunge akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliwaomba wananchi kutoa taarifa pale wanapowaona watu wanaowahisi ni wageni ambao wanaingia wilayani humo bila ya kufuata taratibu hasa wakati huu wa msimu wa mafuno ya mazao ambayo wanakuja kuyanunua kutoka nchi jirani.
Afisa Mtendaji Kata ya Iguguno Josia Pangani akitoa taarifa ya maendeleo ya kata hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh.5 Bilioni kuitekeleza.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida, Msama K. Msama akizungumzia utekelezaji wa miradi ya barabara ambapo Serikali imetoa zaidi ya Sh.19 Biilioni kwa ajili ya kazi hiyo.
Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu (LATRA) Mkoa wa Singida, Layla Daffa akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu viwango mbalimbali vya nauli.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Singida, Onesy Mbembe akizungumzia mikakati ya usambaji umeme mkoani humo.
Kaimu Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mkalama, Kasim Juma akielezea mipango wa kuwafungia umemewateja wapya wa Kata ya Iguguno.
Madiwani wa Kata ya Iguguno wakitambulishwa kwenye mkutano huo. Kulia ni Barnaba Mang'ola na Diwani wa Viti Malumu wa kata hiyo, Mariam Kahola.
Wakazi wa Kata ya Iguguno wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kueleza kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge (hayupo pichani)
Kero zikitolewa.
Mkazi wa Iguguno Wilson Daniel Yindi akitoa kero yake.
Shabani Hamisi akitoa kero yake mbele ya mkuu wa mkoa.
Mkazi wa Iguguno Shabani Sambai akitoa kero yake.
Mohamed Ramadhani akitoa kero yake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Iguguno Kiula Geryson akitoa ufafanuzi wa maaaaambo mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Afisa Elimu Kata ya Iguguno, Stephen Shilla akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Wilaya ya Mkalama, Goodluck Mlau akijibu maswali ya wananchi wa kata hiyo ambao ni wanufaika wa mfuko huo.
Taswira ya mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Sophia Kizigo
amewaalika wawekezaji kwenda kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwamo kilimo
baada ya wilaya hiyo kuanza rasmi uzalishaji wa zao la korosho .
Alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa
ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa
Dk.Binilith Mahenge pamoja na wataalam mbalimbali wa idara za Serikali.
Kizigo alisema wilaya hiyo ambayo awali ilikuwa ikitegemea
mazao ya alizeti,vitunguu, dengu, pamba, mtama na mahindi kama mazao ya biashara sasa imeingia
kwenye kilimo cha korosho ambapo imetenga ekari 200 kwa ajili ya kilimo cha
korosho na kuwa msimu huu wa mazao ndio umekuwa wa kwanza kuvuna zao hilo.
“Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Korosho TARI Naliendele cha
mkoani Mtwara walifanya majaribio ya utafiti wa ardhi kati ya Kongwa mkoani
Dodoma na Singida kuona kama inaweza kuzalisha zao hilo”. Alisema Kizigo.
Alisema baada ya utafiti kubaini wilaya hiyo inafaa kwa
kilimo cha korosho walitenga ekari 200 kwa ajili ya kilimo hichocha korosho na
wananchi kuanza kukichangamkia ambapo alisema korosho hizo ni za ubora wa hali
ya juu na ni I tamu.
Kizigo alisema zao hilo litalimwa kila kata na watafanya
programu maalum ya kuomba kukopeshwa mbegu ili wananchi wengi waweze kulima na
kufundishwa namna ya kulima zao hilo ili waweze kupata fedha na kuweza kulipa
kodi ambayo itaisaidia Serikali kujenga barabara, hospitali, shule na
miundombinu mingine.
Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dk.Binilith Mahenge alisema msimu huu wa kilimo Serikali itatoa mbegu
bora za alizeti aina ya aisuni iliwakulima waweze kulima zaidi na zaidi ambapo
aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo
kuchapa kazi kwa nguvu na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuliletea taifa
maendeleo.
Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu
Hassan inafanya maajabu makubwa ya maendeleo ambapo kwa mwaka mmoja tu Mkoa wa
Singida umepewa Sh.Bilioni 230 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo jambo ambalo lilikuwa halifanyiki kwa miaka
ya nyuma.
Katika hatua nyingine Dk.Mahenge amepiga marufuku tabia ya baadhi ya walimu mkoani humo kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa sababu ya kushindwa kuchangia fedha za malipo kwa walimu wa kujitolea.
"Tunajua kuwa wapo walimu ambao wanajitolea ambao wazazi na walimu mlikubaliana kutoa mchango wa fedha za kuwawezesha mpaka hapo Serikali itakapoweza kupata walimu waajiriwa lakini kukosekana kwa fedha hizo isiwe sababu ya watoto kurudishwa nyumbani sitapenda kuona jambo hilo likitokea" alisema Mahenge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mklama, Asia
Mesos alisema wilaya hiyo walipokea
zaidi ya Sh. 5 Bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikwemo ujenzi wa barabara, shule, vituo vya
afya na Hospitali na maeneo mengine.
Katika mkutano huo watalaam wa idara zote za serikali waliweza
kueleza kazi mbalimbali za miradi ya ya maendeleo zilizofanywa na Serikali na
zinazoendelea kufanyika na kujibu kero zilizoibuliwa na wananchi.
Post A Comment: