Na John Walter-Babati
Mkuu wa wilaya wa Babati Lazaro Twange amesema kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Mratibu wa sensa aliepo sasa kutokana na utendaji wake dhaifu wa kazi katika kuhamasisha watu kushiriki vyema katika sensa ya mwaka huu.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati Twange ameiagiza Halmashauri hiyo kuona hatua zinazofaa kuchukuliwa ila yeye hayupo tayari kufanya kazi na mratibu huyo.
Serikali imepanga kufanya sensa ya watu na makazi ifikapo tarehe 23 Agosti 2022 ambapo kitaifa hufanyika kila baada ya miaka 10 ambapo mara ya mwisho kufanyika sensa ni mwaka 2012 .
Amesema kuwa Sensa ya watu na makazi itaisaidia serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidi mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa .
Pia amesema takwimu sahihi za sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi pamoja na kurekebesha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa katika wilaya ya Babati.
Amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujiandaa kuhesabiwa ifikapo mwezi Agosti na kutoa ushirikiano kwa maafisa watakaokuwa wanapita kuchukua taarifa kwenye maeneo yao.
Post A Comment: