OR - TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa ofisi yake itaendelea kusimamia uwekaji wa mazingira wezeshi ya kufanyia biashara na uwekezaji katika Sekretariti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kustawisha uwekezaji.
Waziri Bashungwa alimuhakikia Mhe. Rais wakati akitoa salamu Juni 9, 2022 kwa niaba ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI katika mkutano wa hadhara wa Mhe. Rais na wananchi katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera
”Mhe. Rais nikuhakikishie tutaendelea kushirikiana na viongozi wenzangu hutasikia Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi baada ya maelekezo ambayo umeyatoa kuhusu suala la uwekaji wa mazingira ya biashara kuwa wezeshi kwa nchi yetu kwenda kinyume na ulivyoelekeza,” amesema Waziri.
Bashungwa amesema, wataendelea kufuata utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuajiri vijana wengi na akina mama nchini waweze kujenga uchumi.
“Mhe. Rais tunaamini uwekezaji wowote ule unaanzia ngazi ya mtaa na kijiji na tupo tayari kutekeleza maelekezo yako," ” amesema Mhe.Bashungwa.
Wakati huo huo Waziri Bashungwa amemuhakikishia Mhe. Samia Suluhu Hassan kutekelezwa kwa maelekezo na maagizo yote aliyoyatoa wakati wa ziara yake mkoani Kagera.
Pia amesema atawaelekeza Mhe. Rais Wakuu wa Mkoa wa Kagera, Kigoma, Katavi, Tabora na Pwani kubainisha maeneo ya ardhi kwa ajili ya kilimo ifikapo tarehe 30, 2022 kama alivyoagiza Rais Samia Suhuhu Hassan.
Amefafanua maeneo hayo yawe yameshabainishwa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Uwekezaji kuhakikisha maeneo hayo yamepatikana kwa ajili ya kuanzisha kilimo ambapo malengo ya nchi ni kujitosheleza katika mfuta ya kula.
Awali, Mhe. Rais wakati akiendelea na ziara yake Mkoa wa Kagera Juni 9, 2022 alielekeza kuwekwe mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.
Amesema, Mkoa wa Kagera una fursa kubwa ya kiuchumi na biashara kwa sababu unapakana na nchi ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo leo Juni, 10 2022 anatarajiwa kufungua msikiti mkubwa mkoani Kagera.
Post A Comment: