Na Mwandishi Wetu
Dar Es Salaam, Mei 2022, Kampuni mashuhuri kwa uuzaji wa bidhaa zinazotumia umeme ya LG Electronics East Africa imetangaza kuzindua Kampeni ya " LGs Something Better " kote nchini inayolenga kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja.
Kampeni hiyo, inatarajia kuendelea hadi tarehe 12 Juni 2022 kwa lengo la kuwapa wateja punguzo la hadi 20% kwa bidhaa zilizochaguliwa pamoja na thamani na manufaa zaidi kwa wateja wanaonunua bidhaa kutoka kwa maduka ya chapa ya LG.Kwa punguzo la ofa, wateja wanatarajiwa kuokoa kuanzia shilingi 50,000/= hadi kufikia Tsh 1,000,000/= katika kipindi cha wiki tano zijazo katika bidhaa zote katika kategoria ya Burudani , Vifaa vya Nyumbani na Viyoyozi vya Makazi.
Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema,
“Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia”.
Hii si tu katika maduka yenye chapa ya LG bali pia katika maduka makubwa ya washirika kama vile Shoppers na Game Super Market.

Kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii kabambe tafadhari tembelea mitandao ya kijamii ya LGs East Africa.
Post A Comment: