Makamu mkuu wa chuo cha Nelson Mandela Prof.Anthon Mshandete akiongea kwa niaba ya mkurugenzi wa huduma za mifugo wa Wizara ya kilimo na mifugo,Profesa hezron Nonga kwenye warsha ya siku moja ya ufunguzi wa mpango wa upimaji na utoaji wa vyeti kwa ugonjwa wa brusela iliyofanyika jijini Arusha.
Awali akiongea wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Mhadhiri wa Shule ya Sayansi ya Maisha na uhandisi wa wanayama Prof.Gabriel Shirima kwenye warsha ya siku moja ya ufunguzi wa mpango wa upimaji na utoaji wa vyeti kwa ugonjwa wa brusela iliyofanyika jijini Arusha
Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI kupitia Wizara ya mifugo nchini imejipanga kuhakikisha Ugonjwa wa Brusela unaoathiri wanyama na binadamu kwa wafugaji na watumiaji wa maziwa yasiosindikwa vizuri au kuchemshwa vizuri ndiyo waathirika wakubwa wa Ugonjwa huo hivyo serikali kujikita kuongeza
bidii ya kukabiliana nao na kuboresha mazao hayo ya mifugo.
Hayo yamesemwa jana na Makamu mkuu wa chuo cha Nelson Mandela Prof.Anthon Mshandete kwa niaba ya mkurugenzi wa huduma za mifugo wa Wizara ya kilimo na mifugo,Profesa hezron Nonga kwenye warsha ya siku moja ya ufunguzi wa mpango wa upimaji na utoaji wa vyeti kwa ugonjwa wa brusela iliyofanyika jijini Arusha.
Amesema Ufugaji wa ngombe wa maziwa kupitia wafugaji wadogo wadogo imekuwa ni sekta inayokuwa kwa kasi ukilinganisha na mifumo mingine ya ufugaji wa ng’ombe. Sekta hii imechangia ajira kwa akina mama na vijana, kuongeza kipato cha kaya, lishe kwa familia na upatikanaji wa mbolea na nishati (Biogas).
Amesema kwamba Ugonjwa huo ni mojawapo ya magonjwa yanayoathiri wanyama na binadamu kupitia njia mbalimbali. Wafugaji na watumiaji wa maziwa yasiyosindikwa au kuchemshwa vizuri ndiyo wanaoathirika zaidi.Ugonjwa huu upo katika mifumo yote ya ufugaji hapa nchini.
“Programu hii imelenga kwenye magonjwa hususani ugonjwa wa Brusela. ni mpango unaohusisha sekta binafsi na serikali katika kutekeleza majukumu yake. Wafugaji wataingizwa kwa hiari kwenye programu hii
ambapo ngombe wao watapimwa nyumba zitakazokuwa hazina Brusela watapewa cheti (Provisional certificate) cha muda wa mwaka mmoja na ikiwa ugonjwa umegundulika basi hawatapewa cheti bali ushauri jinsi ya
kukabiliana na ugonjwa” Amesema Prof. Mshandete.
Awali akiongea wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Mhadhiri wa Shule ya Sayansi ya Maisha na uhandisi wa wanayama Prof.Gabriel Shirima
ameeleza kwamba Baada ya mwaka mmoja cheti kitahuhishwa kwa kupima tena wanyama waliopimwa mwaka uliotangulia. Zoezi hilo litafanyika kwa miaka mitatu mfululizo kabla ya kuwa cheti kamili.
Amesema kwamba ufugaji wa ngombe wa maziwa huchangia ukuaji wa uchumi kwa kaya ajira lishe na unakabiliwa na changamoto za malisho magonjwa na masoko hivyo zoezi hilo limejikita kuandaa sampuli za maziwa katika
vituo kwenye halmashauri za Arumeru na Hai.
Kwa upande wake Prof.Kelvin Mtei Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Utawala Fedha na Mipango Nelson Mandela amsema kwamba uzalishaji wa maziwa kwa
mwaka umekuwa ukiongezeka kwa asilimia 7 toka lita 555 milion mwaka
1995 hadi lita 1.6 blion mwaka 2010.
Alisema sekta hiyo inaweza kukua kwa haraka Zaidi kwa kuzingatia inafuga Ng’ombe wa maziwa katika mazingira Rafiki ikilinganishwa na
idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi Pamoja na ongezeko la ulaji wa bidhaa za maziwa nchini.
Post A Comment: