Muonekano wa Banda la SUA kwene maonesho hayo kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Na Neema Mashingiya, Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kazi nzuri wanazofanya kwa kuandaa vijana na kuwapa elimu inayowawezesha kufanya ubunifu wa vitu mabalimabli pamoja na kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea Banda la SUA kwenye maonesho ya tano ya Mifuko na Program za kuwezesha Wananchi kiuchumi yanayofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
“Kama ikitokea watu wanasema kilimo ni fursa na vijana wakakubali kuingia kwenye kilimo haya maneno tunayosikia hakuna ajira yangekuwa yamekwisha kabisa hivyo niwaombe SUA kuendelea na jitihada hizi kubwa za kutoa elimu bora kupitia wataalamu wake” amesema Mhe.Telack.
Mkuu wa mkoa alitolea mfano wa zao la korosho mkoani Lindi kwa kufafanua kwamba korosho kilo 5 zilizobanguliwa zinatoa kilo 1 ambayo huuzwa kwa shilingi elfu 20,000 mpaka 25,000, Hivyo ukiwa na hekari 3 za korosho tayari wewe ni mwajiri kwahiyo vijana waache kuangalia kilimo kama sio fursa na waanze kutumia taaluma zao kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa mkoa amekitaka Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine kuendelea kutoa elimu kwa Wanafunzi na Wananchi ili kuwasaidia kupata ujuzi zaidi na kuweza kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kililimo biashara na fursa.
Kwa upande wake Juditha Bernad kutoka ushirika wa wahitimu wajasiriamali wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUGECO) ulioanzishwa mwaka 2011, ambao unasaidia vijana kuweza kujiari na kuajiri wengine amesema SUGECO iligundua kwamba vijana wengi wanaosoma masomo ya kilimo wanapomaliza hupata changamoto ya ajira, hivyo ushirika huu unanufaisha vijana kuweza kutumia taaluma zao kwa kujiajiri wenyewe.
Ameeleza namna wanavyonufaika kwa kufanyia kazi yale waliojifunza kwa kutengeneza vitu vyenye ubora kupitia mazao mbalimbali yatokanayo na kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Ameanisha kuwa SEGECO kama ushirika unasaidia vijana hususani wale wanaosoma masomo ya kilimo kuweza kujiamini na kubadili mitizamo yao kwa kuchukulia masomo ya kilimo kama taaluma nyingine kwa kuwafundisha vijana waweze kuona kilimo kama fursa zingine.
“Zipo program nyingi zinazofanyika kupitia wadau mbalimbali pamoja na Serikali kuweza kufundisha vijana kujihusisha na maswala ya kilimo biashara” alisema Juditha.
Naye Mwakilishi kutoka Idara ya Lishe ya Binadamu na Sayansi ya mlaji Athumani Sadala ameeleza namna ambavyo wanatumia mabaki ya vitu visivyotumika kutengenezea bidhaa tofautitofauti kama vile mapipa yasiyotumika kwa kuyakata na kutengenezea makochi,Matairi mabovu ya Baiskeli, bajaji na Pikipiki kutengeneza urembo.
Post A Comment: