Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi Serikali ya mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi katika mitaa ya Kisutu leo Mei 07,2022 jijini Dar es Salaam. Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi gloves kwa wananchi ambao wamefanya usafi katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi fagio kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa vya usafi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) limekabidhi vifaa vya kufanyia usafi katika serikali ya mtaa wa Kisutu pamoja na kujumuika na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Akizungumza katika zoezi hilo leo Mei 07,2022, Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John amesema jukumu lao ni kuhakikisha mji unakuwa safi na salama, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kwa ujumla ili kuona mji unakuwa safi na salama.

"Tukihakikisha mji unakuwa safi na salama hatutaona magonjwa kama kipindupindu na magonjwa mengine ya mripuko, lakini pia miili yetu itakuwa na afya njema na kuongezeka kwa nguvu kazi ambazo ndo tegemezi katika kukuza uchumi". Amesema Bi.Irene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri amewapongeza NEMC kwa kuhakikisha Jiji linakuwa safi na salama ambapo wamepokea vifaa vya kufanyia usafi ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza juhudi kuhakikisha mji unakuwa safi.

Nae Mtaribu wa zoezi la Usafi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa Bw.Moses Mwakiborwa amesema kutokana na Rais wa nchi kuhakikisha anatuletea wageni wa kutosha kuna umuhimu wa mji kuwa safi na salama kwasababu ndo kitovu cha biashara na utambulisho wa nchi yetu.

Amesema zoezi hilo la kufanya usafi kwao litakuwa ni endelevu mpaka watakapohakikisha jiji linakuwa safi na salama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama walivyofanya leo NEMC.

Pamoja na hayo NEMC imetoa wito kwa taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kuhakikisha wanafanya kila namna ili kuhakikisha jiji linakuwa safi na salama maana hii ni njia ya kuunga juhudi za Serikali la kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: