Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Gerson
Msigwa akizungumza wakati wa ziara ya Maafisa Habari wa Wizara na Taasisi za Umma
nchini katika Bandari ya Tanga ambao wapo Jijini Tanga wakiendelea na
kikao chaoSehemu ya Maafisa Habari wa Wizara na Taasisi za Umma wakiwa kwenye Bandari ya Tanga wakati wa ziara hiyo
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
SERIKALI ipo na mazungumzo na wawekezaji juu ya mpango wa ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo mkoani Pwani ili kusogeza huduma karibu na wananchi na hivyo kuchangia kukuza pato la Taifa na wananchi kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Gerson Msigwa wakati wa ziara ya Maafisa Habari wa Wizara na Taasisi za Umma nchini katika Bandari ya Tanga ambao wapo Jijini Tanga wakiendelea na kikao chao
Alisema kwa sasa wamerejesha mazungumzo hayo baada ya Rais Samia Suluhu kupitia serikali yake
ya awamu ya sita kuona ni vyema wakarejesha mazungumzo hayo na
kukubaliana maeneo serikali itayoona ina maslahi nayo pamoja na
wawekezaji ili wautekeleze mradi huo.
Alisema
huo mradi huo ni mkubwa na wakifanikiwa kuutekeleza utasaidia
kuchochea kasi ya maendeleo na hivyo kuchangia pato la wananchi na Taifa
kwa ujumla ikiwemo kufungua milango ya uwekezaji hapa nchini.
Alisema
sio Bandari bali patajengwa Viwanda, kwasababu eneo hilo wanakusudia
kulifanya liwe kanda maalumu ya kiuchumi ya Bagamoyo pale panajengwa
bandari, Viwanda, eneo la makazi ,maduka makubwa na sehemu nyingi za
kibiashara ikiwemo ujenzi wa viwanda takribani 1000 na hivyo itawezesha
kuwa kanda maalumu ya viwanda.
Akizungumzia
ujenzi wa Bandari unaoendelea katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na
Mtwara Msigwa alisema wamewapeleka maafisa habari wa serikali ili waone
kazi kubwa inayotekelezwa na serikali ili wananchi wanapotaka kujua nini
serikali inafanya katika fursa ya uchumi wa bluu ili wajue kwamba kuna
kazi kubwa inayofanyika.
"Niwaambie kwamba hii moja kati ya kazi kubwa ambazo zinafanyika hapa Tanga lakini pia
tunafanya kazi kama hizi kwenye maziwa yetu ikiwemo Kigoma, Kalema kule
kwenye ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria pia pale Mwanza tumejenga cholezo
kubwa na ujenzi wa meli unaendelea kule kwa hiyo kuna kazi nyingi
serikali inafanya,kwenye maeneo haya na tungependa maafisa habari wetu
wajionee wao wenyewe na kupeleka huu ujumbe mzuri kwa wananchi,
"Alibainisha Msigwa.
Akizungumzia
miundombinu ya reli Msigwa alisema serikali imefanya kazi kubwa ya
kuhakikisha treni zinarejea Mkoani Tanga mpaka Arusha ambapo hivi sasa
kazi inayokwenda kufanyika ni ya kuimarisha miundombinu hiyo na kuona
namna bora ya kuja na reli nzuri zaidi.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mhandisi
wa bandari ya Tanga Hamis Omari Kipalo amesema kwa upande wa ujenzi wa
gati namba moja na namba mbili katika bandari hiyo umefikia asilimia 45
mpaka sasa.
Mhandisi huyo alisema mradi wao kimkataba unatakiwa kukamilika tarehe 16 mwezi octoba mwaka huu.
Baadhi
ya maafisa habari waliotembelea bandarini hapo wamesema ziara hiyo
imewasaidia kuona namna serikali ilivyojizatiti kwenye utekelezaji wa
miradi mikubwa ya maendeleo.
David
Mwaipaja ni Afisa mahusiano na mauzo kutoka Watumishi Housing
Investment amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika
bandari zetu ambazo zipo kwenye miradi ya kimkakati jambo ambalo
litakuwa chachu kwa maafisa habari kuchukua na kwenda kuisemea serikali
kwa wananchi ili mambo yasiyoonekana kiurahisi kwa wananchi basi yaweze
kuwafikia sawasawa na serikali inavyofanya.
Upanuzi
wa ujenzi wa mradi wa gati za kisasa katika bandari nchini unatarajiwa
kufungua fursa za kibiashara ambapo ujenzi huo umefanyika katika Mikoa
ya Tanga, Mtwara na Daresalaam.
Kwa
upande wa bandari ya Daresalaam jumla ya shilingi trilioni moja nukta
mbili zinatarajiwa kutumika kwajili ya ujenzi wa gati sambamba na
kununua vifaa vitakavyorahisisha utoaji wa huduma ikiwemo upakuaji wa
shehena.
Post A Comment: