Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema kwa sasa hakuna nafasi nyingine kwa waliokuwa makada 19 wa chama hicho ya kukata rufaa. Pia, amesema hatua inayofuata ni Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuandika barua ya kumtaarifu Spika wa Bunge kuhusu uamuzi uliofanywa na baraza kuu kwa hatua zaidi ikiwemo ya kutangazwa kuvuliwa ubunge.
Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ni uhuni.
Post A Comment: