Jumla ya watahiniwa 4124 Leo wameanza mitihani ya kidato Cha sita na ualimu mkoani Arusha katika Halmashauri 7 na nchini ambapo maandalizi yote kwa mkoa yamekamilika.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athman Kihamia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya mitihani mkoa Amewataka watahiniwa kufuata maelekezo ya mitihani ili kuendelea kuupaisha mkoa huo.
Amesema kwamba mitihani hiyo imeanza tarehe 9 mei hadi Mei 27 mwaka huu kwa maandalizi yote kufanyika ikiwemo kuwaandaa watahiniwa kupokea na kusambaza vifaa vya mitihani kuteua wasimamizi na kuendesha semina
Aidha amebainisha kwamba ikiwemo ukaguzi wa vituo pia kuandaa ulinzi wa mitihani na vituo vya kufanyia mitihani,ambapo tunaipongeza serikali kwa kutoa pesa kiasi Cha Milion 347,568,000 za uendeshaji wa zoezi hilo la mitihani ya kidato Cha sita na ualimu na hakuna changamoto yeyote iliyojitokeza hadi sasa.
Akiongelea vituo na watahiniwa wa mitihani Dkt.Kihamia amesema idadi ya watahiniwa wote wa mitihani ya kidato Cha sita wa shule na wakujitegemea ni 4124 wa shule 3701 na wakujitegemea 423 watahiniwa wa ualimu ni 456.
Amebainisha vituo vya mitihani Jumla ni 49 na vituo vya mitihani ya ualimu ni vinne ambapo idadi ya wasimamizi wa mtihani wa kidato Cha sita 121 na ualimu 12 huku waandaaji wa mitihani ya vitendo ni 111
Amewatahadharisha watahiniwa kutojiingixa kwenye vitendo vinavyoweza kutafsiriwa kuwa ni uhujumu wa zoezi la mitihani kwa muda wote wa zoezi hilo ukiendelea ikiwemo kutothubutu kuingia kwenye vyumba vya mitihani na vituo walivyokatazwa.
Akatoa wito kwa wasimamizi wote kutanguliza uzalendo na uadilifu kama walivyokula kiapi Cha kutunza Siri za mitihani wawe watulivu kuepuka papara zinazoweza kuathiri utaratibu mzima uliowekwa wa ufanyikaji wa mitihani hiyo.
Post A Comment: