![]() |
![]() |
Na John Mapepele.
Serikali
ya Tanzania na China leo, Mei 26, 2022 zimetiliana Saini mkataba wa
makubaliano ya kusaidiana katika kuboresha maeneo ya Sekta
anazozisimamia.
Utiaji wa
Saini wa mikataba hiyo ya kihitoria umeongozwa na Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo. Mhe. Mhamed Omary Mchengerwa kwa upande wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi wa China nchini Wang Ke kwa
upande wa Serikali ya watu wa China kwenye Ofisi ya Ubalozi wa China
jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
kuhusiana na manufaa ya mikataba hiyo, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali
ya Tanzania imesaini mikataba hiyo ya ushirikiano inatarajia kuleta
mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo.
Amesema
kwa upande wa utamaduni kutakuwa na kupeleka wadau wa utamaduni,
sanaa na michezo katika nchi ya china na watu wa china kuja nchini kwa
ajili ya kubadilishana uzoefu.
Kwa
upande wa elimu Tanzania itapeleka wanafunzi ambapo China itafadhili
masomo haya kwa kutoa nafasi 120 kwenda kwenye maeneo ya lugha,
utamaduni, sanaa na maeneo mengine ya hinsia (humanities) kila mwaka
ambapo Tanzania itatoa ufadhili wa nafasi 15 kwa ajili ya wachina kuja
Tanzania kusoma hasa kwenye maeneo ya hinsia(humanities) pamoja na
maeneo ya lugha.
Aidha,
amesema mkataba huu unatarajiwa kutoa nafasi kwa wataalam kwenye
maeneo ya sekta hizo zote. Pia imeelezwa kuwa Serikali ya China
inatarajia kujenga vituo vya kisasa vyenye miundombinu yenye viwango vya
kimataifa vya sanaa na utamaduni ambavyo vitatumika na wasanii wa
hapa nchini katika kuzalisha kazi zao zenye ubora ambazo zitauzwa
duniani.
“Ni
jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa wasanii wetu wanakwenda kupata
studio za kisasa kabisa kwa ajili ya kuzalisha kazi zao”amefafanua
Mhe. Mchengerwa.
Aidha,
amesema Tanzania inaamini kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na utamaduni
uliosheheni vitu vingi kutokana na kuwa na makabila ambayo ni zaidi ya
120.
Amesema kulingana na
mikataba hiyo Serikali za nchi zote zinakusudia kuchangamsha utamaduni
na sanaa ili ziwe kwenye kiwango halisi tofauti na sasa ambapo
inaonekana kuwa kutochangamka kwa kiwango hicho.
Katika
ziara hiyo Waziri Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi na Wakurugenzi wa Sekta za
Utamaduni na Sanaa kwenye Wizara hiyo, ambapo kwa Serikali ya China Mhe.
Balozi Wang Ke ameambatana na watendaji waandamizi kwenye sekta hizo.
Post A Comment: