Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)inayoongozwa na Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji imeungana na asasi nyingine kushiriki na kuyapamba mashindano ya Tulia Trust Marathon 2022 katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


Akimwakilisha Mkurugenzi wa Taasisi Diwani wa Kata ya Mbalizi Road Adam Simbaya amesema lengo la kushiriki ni kuimarisha afya zao sambamba na kuchangia mfuko kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu kupitia Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini.








Share To:

Post A Comment: