Benki ya Equity Tanzania Katika muendelezo wa kuhakikisha wapo karibu na jamii mapema leo walipata fursa ya kutembelea vituo vya kulea watoto yatima vya Ijango Zaidia-Sinza,Faraja Orpahange-Mburahati na Zimamu Salikiin-Tandika ili kuwajulia hali, kutambua changamoto wanazopitia na kuwapatia mahitaji yao muhimu.
“Tumeguswa na watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima kikiwamo kituo hiki, ndiyo maana tumekuja kutoa msaada huu ili kufanikisha kusherehekea pamoja sikukuu hizi mbili na kuondokana na hali ya kuona kama mmetengwa na jamii,”Alisema Mwakilishi wa Benki ya Equity alipokuwa akikabidhi Msaada huo.
Baadhi ya Watoto walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Equity Tanzania waliofika kukabidhi msaada katika kituo hicho .Jukumu la kuwasaidia watoto yatima ,na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi na magumu inahitaji nguvu ya pamoja kwa kushirikiana na jamii pamoja na wadau ili kunusuru changamoto zinazowakabili watoto hao
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Equity Tanzania wakiwa Katika picha ya Pamoja mara baada ya kukabidhi Msaada katika vituo vya kulea watoto yatima vya Ijango Zaidia-Sinza,Faraja Orpahange-Mburahati na Zimamu Salikiin-Tandika mapema leo Jumamosi tarehe 7 Mei 2022,Jijini Dar Es salaam.
Post A Comment: