Na Mustafa Leu
TEKNOLOJIA ya kuunganisha vikonyo vya miche ya mibuni chotara ya Arabica na Robusta mkombozi kwa mkulima wa zao la Kanawha
Mtaalamu wa uchumi na kilimo kutokaTaCRI Leonard Kiwelu,anasema wanatumia teknolojia ya kuunganisha miche ya mibuni kwa kutumia njian ya vikonyo na kupata mbegu bora za chotara ambazo zina zaa sana,zinahimili magonjwa na wadudu
Amesema kutokana na matumizi ya teknolojia hiya kumeiwezesha nchi yetu kuwa ya 8 ulimwenguni na ya tatu barani afrika kwa kuzalisha kahawa yenye ubora na viwango vya kimataifa.
Kutokana na mafanikio hayo tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) imeitunuku TaCRI,shilingi milioni 20 kutokana na ongezeko la uzalishaji wa Kahawa
Anasema matumizi ya teknolojia kwenye kilimo imeongeza mavuno na thamani ya kahawa na hivyoTaCRI, imeweza kuzalisha miche milioni 51,323,308 ya mibuni na tayari wakulima na tayari wakulima 377,496 wameshanufaika na mafunzo ya teknolojia hiyo
TaCRI,Iliyoanzishwa miaka 20 iliyopita kwa ajili ya kufanya utafiti wa zao la kahawa imeanzisha bustani 400 za miche ya mibuni na imetoa mafunzo ya teknolojia ya uzalishaji miche bora ya mbegu chotara kwa maafisa ugani108,65 nchini.
Taasisi hiyo imeanza kuhamilisha tafiti za magonjwa na vinasaba lengo ni kuendeleza uhakiki, uzalishaji na usambazaji wa wa aina ,mpya za Kahawa ambazo ni Arabika na Robusta
Post A Comment: