Na,Joel Maduka
Chama cha Mapinduzi CCM kinaheshimika na kufahamika kwa mfumo wake mzuri wa demokrasia iliyoshamiri ndani yake, kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwake baada ya kuungana kwa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini ASP kwa Zanzibar na TANU kwa Tanzania bara 1977 vijana wamekua ni nguzo imara ya kushamirisha demokrasia kwa kuaminika kuwa Tanuru mahsusi la kuoka na kuzalisha viongozi katika njanja mbalimbali za uongozi ndani ya Chama lakini pia Serikalini.
Kuna msemo maarufu usemeao “usipoongoza basi utaongozwa”. Muda umefika, kipyenga kimeshapulizwa, zoezi la kuchukua fomu maeneo yote nchini linaendele ni wakati wetu vijana kuchangamkia fursa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zilizoanishwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Kanuni za umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Vijana hatupaswi kubaki nyuma na kubweteka ni wakati sahihi kwetu vijana kujitokeza kwa wingi, kuchukua, kujaza, na kurejesha fomu za uongozi ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa , kuonyesha vipaji na uwezo wa uongozi uliopo ndani ya Vijana huku tukisimamia kauli mbiu ya uchaguzi isemayo ‘Chama Imara Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu’.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati anaongea na vijana Jijini Mwanza Tarehe 15 June 2021 alisema “vijana ni engine ya maendeleo kwa Taifa lolote lile na Taifa lolote ulimwenguni haliwezi kuendelea bila kuwatumia vijana wake”. Hii inatuamsha vijana na kuiona thamni yetu katika Taifa letu la Tanzania kwa kuona ni jinsi gani mwenyekiti wa chama chetu anatambua umuhimu wa uwepo wa vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na hata nje ya Chama kwa maendeleo ya Taifa letu.
Nafasi za kugombea uongozi ndani ya UVCCM ni nafasi za vijana kwa mujibu wa katiba ya CCM na kanuni za UVCCM, hivyo ni jukumu letu vijana kujitokeza na kugombea nafasi zote za uongozi zilizoanishwa kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa.
Ratiba ya uchaguzi ndani ya UVCCM ni kama ifuatavyo (1) Tarehe 3-10/04/2022 kuchukua na kuresha fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea uongozi wa UVCCM kwa ajili ya michakato mingine ngazi ya Tawi, Tarehe 26-29/05/2022 kuchagua viongozi wa Jumuiya ya uymoja wa vijana ngazi ya Tawi. (2) Tarehe 4-11/06/2022 kuchukua na kuresha fomu kwa ajili ya michakato mingine ngazi ya Kata/Wadi, Tarehe 14-17/07/2022 kuchagua viongozi wa UVCCM ngazi ya Kata/Wadi. (3) Tarehe 2-10/07/2022 kuchukua na kuresha fomu za kuomba uongozi wa UVCCM kwa ajili ya michakato mingine ngazi ya Wilaya/Jimbo, Tarehe 19-21/08/2022 kuchagua viongozi wa UVCCM Ngazi ya Wilaya/Wadi (4) Tarehe 4-10/07/2022 kuchukua na kurejesha fomu za maombi ya uongozi katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ngazi ya mkoa Tarehe 06-09/10/2022 kuchagua viongozi wa UVCCM ngazi ya Mkoa. (5) Tarehe 04-10/07/2022 kuchukua na kurejesha fomu za uongozi ktika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ngazi ya Taifa na Ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, uwakilishi wa UVCCM, Tarehe 04-06/11/2022 kuchagua Viongozi wa Jumuiya ngazi ya Taifa wakiwemo wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa.
Zipo nafasi nyingi sana za kugombea uongozi ndani ya UVCCM kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa hivyo nawasihi sana vijana wote nchini waliotimiza vigezo na kujipima kwa uwezo wao kujitokeza kwa wingi kugombe nafasi zote ndani ya umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwani hakuna mtu yoyote nje ya Vijana anayeweza kuchukua nafasi hizo kama nilivyoeleza awali kuwa upekee wa nafasi za uongozi ndani ya UVCCM ni nafasi za Vijana pekee tofauti na ndani ya CCM, UWT na Jumuiya ya Wazazi ambapo nafasi za uongozi huko ni kwa mwanachaa yoyote aliyekizi vigezo vya kikatiba na kikanuni ana haki ya kugombea nafasi hizo.
Sanjari na hilo ni lazima vijana tuwe waadilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuichafua taswira halisi ya uchaguzi ndani ya UVCCM, Jumuiya y Umoja wa Vijana wa CCM kwenye chaguzi zake tangu kuanzishwa kwake imekua ni mfano wa kuigwa kwa kupinga vitendo ya kubebana, Rushwa, na kujuana hali inayopelekea kupatikana kwa viongozi makini, na hodari ambao wanabeba maono na mahitaji halisi ya vijana katika Taifa letu. Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kilelele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Januari 07, 2022 alitausa vijana kuwa makini katika chaguzi mbalimbali kwa kusema “ Vijana msitumike kukipasua Chama nendeni kakiimarisheni Chama na Jumuiya yenu, vijana msitumike vibaya”. Lakini pia akaenda mbali kwa kusema “ Uzoefu unaonyesha kuwa vijana mnageuzwa ngazi na kuwabeba watu wanaotaka uongozi kwa tama za fedha na ahadi za uongozi, mjiulize kama hao mliowabeba wangeonyesha utendaji mzuri leo hii msingekua na changamoto mnazozisema”.
Kwa kauli hizi za Mwenyekiti wetu na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan zinatuamsha vijana kuongeza umakini kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ndani ya CCM na Jumuiya yetu ya Umoja wa Vijana wa CCM kwa kuhakikisha hatushiriki katika vitendo vyovyote vile vya kuwabeba wagombea wala kutoa au kupokea rushwa kwa kigezo cha kumpigia kura au kumnadi mgombea flani na hapo ndipo tutakua tumishi kwenye kauli mbiu ya uchaguzi mkuu ndani CCM ya mwaka 2022 ‘Chama Imara, Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu’.
Post A Comment: