MINYOO kutumika kwa ajili ya kuboresha rutuba ya udongo mashambani na kuongeza uzalishaji wa mazao utafiti umebaini ina faida kubwa hasa kwa wakulima wa zao la kahawa.
Minyoo ni jamii ya wadudu ambayo inwonekana kutokuwa na thaman hivyo hawatiliwi uzito lakini sasa wanasayansi wamefanya utafiti na kugundua kuwa ni wadudu mhimu katika kuboresha rutuba ya udongo mashambani.
Mtafiti mwandamizi wa udongo mashambani wa kituo cha utafiti wa mbegu za kilimo na mazao cha Seliani,Richard Temba,anasema kituo kinatumia teknolojia kufanya utafiti wa minyoo ambayo inazalishwa kutokana na maganda ya kahawa.
Anasema utafiti uliofanywa duniani umegundua kuna aina 400 za minyoo kati yake aina10 zina uwezo wakuchakata mbolea mashambani na kuongeza rutuba ya udongo na mazao mashambani.
Minyoo hiyo hubadilisha taka na kuwa ni mbole ambayo ni chakula cha mimea na mazao hivyo wakulima wa zao la kahawa watakuwa ni wanufaika wakubwa wa teknolojia hiyo wakulima wengi wamekuwa hawaelewi manufaa yanayotokana uwepo wa minyoo kwenye mashamba Yao.
Utafiti wa udongo na minyoo,unafanywa kutokana na ufadhili kutoka Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia,COSTECH,ambapo Teknolojia hiyo itamwezesha mkulima kupata mazao mengi na kuondoka kwenye kilimo cha mazoea.
Temba,anasema,mbali,na utafiti wa minyoo pia taasisi hiyo inafanya urafiti wa udongo kwa kupima sampuli kwa ajili ya kuleta mapinduzi kwenye kilimo teknolojia ambayo inawezesha wakulima kuongeza uzalishaji
teknolojia hiyo ya utafiti wa udongo itatumika kupima udongo wa mashamba kwenye maabara ili kuangalia ubora na rutuba ambapo matokeo ya upimaji huo yatawawezesha kufahamu aina ya udongo na rutuba na mazao wanayoweza kuzalishwa na aina ya mbolea inayofaa
Post A Comment: