Na Mwandishi Wetu.

Mtandao unaoongoza kwa mageuzi ya Kidigitali hapa nchini Tanzania , Tigo Tanzania ukishirikiana na Kampuni ya Simu ya TECNO leo Aprili 01, 2022 wamezindua simu mpya ya Tecno Spark 8 yenye uwezo mkubwa zaidi na huku ikiwa na GB 78 BURE kutoka Tigo kwa Mwaka mzima.



Akizungumza katika uzinduzi Wa Simu hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Kampuni ya Tigo Bi. Woinde Shisael amesema kuwa 

" Tigo siku zote tunawaletea Watanzania kilicho bora na ndio maana leo hii tumeshirikiana na kampuni ya simu ya Tecno Tanzania kuwalete a simu bora ya TECNO SPARK 8 ili uweze kufurahia maisha ya Kidigitali popote ulipo huku ukiwa na Ofa ya Intaneti ya GB 78 BURE kutoka Tigo kwa Mwaka Mzima , hii ni kutokana na mapenzi tuliyonayo tigo kwa wateja wetu kote nchini na ndio maana siku zote tunakua msitari wa kwanza kuwaletea Watanzania kilicho bora na kupaisha mageuzi ya Kidigitali nchini Tanzania". 



Kuwa wa kwanza kununua Tecno Spark 8 , ufurahie Maisha ya kidigitali , Kumbuka simu hii imekuja na Promosheni ya kushinda Milioni 5 utakapoinunua kutoka katika maduka ya Tigo na Tecno nchini kuanzia leo April 01 - 30 mwaka huu." Alimalizia Bi Woinde.

Naye kwa upande wake Mwakilishi kutoka kampuni ya simu ya TECNO Bi. Joyce J. Kaswalala amesema kuwa 


" Simu hizi za Tecno Spark 8 zitapatikana kwa bei ya Tsh. 290,000 pamoja na 240,000 katika maduka ya Tigo na Tecno kote nchini , nawasihi wateja wetu wachangamkie fursa hii ili waweze kujishindia pesa Taslimu na Ofa nyingine kibao kutoka kwa Tigo na Tecno ".

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: