Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dk. Geoffrey Mkamilo anesema,TARI inaendelea kuwekeza kwa nguvu katika usambazaji wa teknolojia na kutumia vyombo vya habari kusambaza habari mbali mbali za tafiti za kilimo.


Dk. Mkamilo ameyasema hayo leo katika kikao kazi cha viongozi Wakuu wa Idara na vituo 17 vya Taasisi hiyo.


Dk. Mkamilo amesema kuwa Taasisi imepata mafanikio ya usambazi wa teknolojia za kilimo kupitia vyombo vya habari. 


Dk. Mkamilo aliwataka Wakurugenzi na Mameneja wa Vituo kuwekea umuhimu katika kuhakikisha kuwa Usambazaji wa Teknolojia kupitia njia mbalimbali za Mawasiliano unasimamiwa kikamilifu.

Share To:

Post A Comment: