Na John Walter-Babati
Serikali imesema imepanga kutengeneza Barabara ya Babati-Galapo hadi Orkesmet wilayani Simanjiro kwa kiwango cha lami fedha zitakapopatikana.
Akijibu swali la Daniel Sillo Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Bungeni jijini Dodoma leo April 8,2022, naibu waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema barabara hiyo ni muhimu na tayari imeshafanyiwa ufanisi wa kina.
Mheshimiwa Sillo aliuliza "ni lini serikali itaanza kujenga bara bara ya Babati-Galapo hadi Orkesmet kwa kiwango cha lami"?
Kasekenya amesema serikali inaendela kutafuta fedha ili bara bara hiyo ianze kujengwa kwa kiwango cha lami.
"Mheshimiwa Spika mara baada ya serikali kupata fedha bara bara hiyo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami" alisema Naibu waziri.
Ujenzi wa miundombinu ya barabara hiyo kwa kiwango cha lami itafungua maeneo hayo kibiashara na kuchochea fursa nyingi za kimaendeleo katika mkoa wa Manyara kwa kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kirahisi.
Post A Comment: