Na John Walter-Babati
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, mhe Pauline Philip Gekul ameipongeza timu ya soka ya Simba kwa kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kibabe kwa kuichapa bao 4-0 US Gendamerie mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mhe Gekul akizungumza leo Jumatatu april 4 akifungua mashindano ya kusaka timu ya riadha ya mkoa wa Manyara katika kata ya Maisaka mjini Babati yaliyofanyika katika shule ya sekondari Kwang.
Gekul amewataka mashabiki wa timu za Yanga na zingine kuungana kuishabikia Simba Sc kwa kuwa inapeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.
Amesema inapotokea timu inacheza kuliwakilisha taifa ni wakati wa kuweka ushabiki pembeni.
"Niwaambie kabisa wananchi mimi sina timu,wote ni wa kwangu,kwenye wizara tunalea michezo zaidi ya 78,wenzetu wa simba jana walikuwa wanajenga heshima ya nchi"alisema Gekul
Mbali na Simba kutoka Tanzania pamoja na RS Berkane kutoka Morocco ambazo hizi zipo kundi D pia zipo nyingine ambazo ziliweza kutinga hatua ya roo fainali.
Timu hizo ni pamoja na Al Ahly Tripoli ya Libya na Pyramids ya Misri hizi zilikuwa kundi A.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini na A Ittihad ya Libya kutoka kundi B.
TP Mazembe ya DR Congo na Al Masry ya Misri kutoka kundi C.
Jumanne April 5,2022 inatarajiwa kuchezwa droo ya mechi za robo fainali na Simba inaweza kukutana na Al Ahly Tripoli, Orlando Pirates au TP Mazembe ambazo zimemaliza vinara katika makundi yao.
Post A Comment: