Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe.Jumanne Sagini akiendesha baiskeli katika uzinduzi wa Msafara wa Baiskeli kutoka Mikocheni Jijini Dar es Salaam hadi Butiama mkoani Mara. Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe.Jumanne Sagini akizungumza wakati wa uzinduzi wa Msafara wa Baiskeli kutoka Mikocheni Jijini Dar es Salaam hadi Butiama mkoani Mara. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Godwin Gondwe akizungumza katika uzinduzi wa Msafara wa Baiskeli kutoka Mikocheni Jijini Dar es Salaam hadi Butiama mkoani Mara. Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza katika uzinduzi wa Msafara wa Baiskeli kutoka Mikocheni Jijini Dar es Salaam hadi Butiama mkoani Mara. Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe.Jumanne Sagini akiwa pamoja na Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi wa taasisi za Maliasili na utalii wakipata picha ya pamoja na waendesha Baiskeli wa Klabu ya TWENDE BUTIAMA katika uzinduzi wa Msafara wa Baiskeli kutoka Mikocheni Jijini Dar es Salaam hadi Butiama mkoani Mara. Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe.Jumanne Sagini akizindua Msafara wa Baiskeli wa TWENDE BUTIAMA leo katika makazi ya zamani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Hayati Julius Kambarage Nyerere waendesha baiskeli wa klabu ya TWENDE BUTIAMA wanatarajia kuanza msafara wa baiskeli kutoka Masaki Jijini Dar es Salaam kama kutoa ujumbe kwa jamii kuenzi na kukumbuka na kufanya utathimini wa urithi wa wazee wetu waliotuachia.

Akizungumza katika uzinduzi wa msafara huo leo Jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Jimbo la Butiama, Mhe.Jumanne Sagini amesema kuna umuhimu mkubwa wa kumuenzi Baba wa Taifa kwani ni mengi mema ameyafanya kwenye Taifa hili.

Amesema Watanzania wanatakiwa kutumia maadhimisho haya kuungana kwa pamoja katika kuhakikisha wanatangaza vivutio vya nchi yetu yetu kama vile alivyokuwa anafanya Mwalimu Nyerere.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John amesema wameamua kushiriki tukio la kuenzi yale yote ambayo ameyafanya baba wa Taifa kwasababu alikuwa ni muhifadhi namba moja wa vivutio vya Utalii nchini ambavyo tunaendelea kuvitangaza duniani kote.

"Kupitia programu ya TWENDE BUTIAMA, TTB inahamasisha Utalii wa ndani pamoja na kutangaza Utalii wa Kikanda kwa maana katika bara la Afrika hivyo watanzania wanatakiwa kuenzi yale yote ambayo Baba wa Taifa ameyafanya". Amesema Bw.John.

Nae Mwenyekiti wa Klabu ya TWENDE BUTIAMA,Bw. GABRIEL LANDA amesema wameamua kutumia baiskeli katika msafara kwasababu Nyerere alikuwa anatumia baiskeli katika shughuli zake.

Amesema msafara huo wa baiskeli unashirikisha Watanzania kutoka maeneo mbalimbali lakini pia wanawaendesha baiskeli wenye umri mdogo na mkubwa pia unajumuisha rika zote yaani wakike na wakiume.

Vilevile amesema katika msafara wataanzia Mikocheni Jijini Dar es Salaam tarehe 7 na kupumzikia Gairo, tarehe 8 wataanza safari mpaka Itigi watapumzika, tarehe 9 wataanza safari mpaka Nzega , tarehe 10 wataendelea mpaka Magu na tarehe 11 watamalizia safari mpaka Butiama.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: