Mkurugenzi wa Kampuni ya Mo Green International Bw. Matolo Patrick akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitambulisha bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo kazi yake kuuwa wadudu wanaoshambulia zao la pamba. Afisa Kilimo wa Kampuni ya Mo Green International , Bw.Alex Michael akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitambulisha bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo kazi yake kuuwa wadudu wanaoshambulia zao la pamba.
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Mo Green International inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo nchini imezindua bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo ni kiuadudu ambacho kinauwezo wa kuuwa wadudu wa kufyonza na kukata kwenye pamba na mazao mengine.
Akizungumza leo Aprili 8,2022 na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mo Green International Bw. Matolo Patrick amesema kiuwatirifu hicho kinaua kwa kiasi kikubwa kwani kiambata chake cha LAMDACYHALOTHRIN 101g/I+THIAMETHOXAM 141g/I ni bora ndani yake.
Amesema kwenye zao la pamba kuna matatizo mengi hasa ya wadudu mbalimbali, kuna wadudu wanaokata au kutafuna mazao na kuna wadudu wanaofyonza pamba na kusababisha pamba kwenda kwenye gredi ya pili badala ya kwenda kwenye gredii ya kwanza.
"Hawa wadudu wanasababisha mkulima kupunguza mapato kutoka asilimia 70 mpaka 90, kwahiyo kampuni yetu ipo kwaajili ya kumlinda mkulima wa pamba sehemu hiyo". Amesema.
Aidha amesema lengo kubwa la kampuni hiyo ni kushirikiana na wakulima kuhakikisha wakulima wanapata mafunzo sahihi kwenye utumiaji wa viuatirifu na kwenye kulinda mazao yao ili kuongeza kipato na kupata mazao yaliyo bora zaidi.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kampuni ya Mo Green International , Bw.Alex Michael amesema dawa ya Mp Strong inauweo mkubwa wa kuangamiza wadudu ambao wanashambulia pamba hivyo wanavipimo ambavyo wameviweka kwaajili ya kutumika kwa mkulima anetumia kupambana na hao wadudu.
"Tumeweka vipimo ambapo mtu akitumia bomba lenye ujazo wa lita 16 tunashauri atumie miezi 15 mpaka miezi 20 na kwa yule ambaye atakuwa anatumia bomba la lita 20 yeye tutashauri apime miezi 19 mpaka miezi 24". Amesema
Post A Comment: