MKEMIA mkuu ni kikwazo cha mtafiti kupata mafanikio ya tafiti zake na kusababisha bidhaa anazozalisha kushindwa kuwepo kwenye masoko na kushindwa kupata mafanikio na malengo ya ufafiti wake.
Kwa kipindi cha miaka 40 ya utafiti pamoja na kuwasilisha matokeo ya tafiti zake ofisi ya Mkemia mkuu imeshindwa kutoa Kibali cha kuidhinisha kwa dawa zilizofanyiwa utafiti kwa kutumia teknolojia ili ziingie kwenye soko.
Hali hiyo inamfanya mtafiti Salvatory Rwebangira,mwenye umri wa miaka( 72) analazimika kusubiri mamlaka husika ili iweze kuidhinisha dawa zake anazozalisha bila kutumia kemikali ili ziweze kuingia kwenye masoko na kutumika kutibu magonjwa mbalimbali..
Amesema kuwa miaka 40 imepita tangia aanze kufanya utafiti wa dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ameambulia kutunukiwa cheti cha kutambuliwa dawa zake kutoka Muhimbili Medical research lakini hakimwezeshl kupeleka dawa zake kwenye masoko mpaka apate kiballi toka kwa mkemia mkuu wa serikali..
Rwebangira,anasema kuwa mara baada ya yakukamilisha tafiti za dawa ambazo anaamini zina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali miaka michache iliyopita aliwasilisha aina 30 tafiti zake kwa mkemia mkun na. taasisi ya utafiti wa tiba asili taa mhimbili ili wazipitie na hatimae ziidhinishwe bado hajakata tamaaa.
Anasema ametengeneza mafuta yanayotokana na wanyama ,miti, asali ,na ametengeneza sabuni,alianzisha maabara yake inayotembea mjini Mwanza ,ambayo sasa ameihamishia nyumbani kwake maeneo ya uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.
Anasema safari yake ya utafiti wa dawa ilianza mwaka1977 baada ya Wazungu waliokuwepo nchini wakifanya kazi na kaka yake walipokutana nae na kumshauri kaka yake ampeleke nchini Uganda kufundishwa utafiti wa dawa na madini mafunzo ambayo yalimchukua miaka minne.
Anasema alipokuwa shuleni hakuwahi kuwa na wazo la kuwa iko siku atakuwa mtafiti ,wazo hilo lilikuja kutokana na kuhamasishwa na wazungu ambao walikuwa ni rafiki wa kaka yake waliokuwa wakifanya nae kazi ya utafiti ambao baada ya kumuona na kuhojiana nae waligundua kuwa ana kipaji cha kufanya utafiti
Anasema ana uwezo wa kuzalisha vikinga maambukizi ya ugonjwa wa Uviko19 (Santizer,) za kutosheleza mahitaji ya nchi nzima bado anasubiri kibali cha mkemia mkuu wa serikali
Post A Comment: