Na,Jusline Marco;Arusha
Kaimu Mkuu, Mkoa wa Arusha Frank Mwaisumbe amelitaka shirika la viwago Tanzania kuongea juhudi katika kuainisha viwango ngazi ya kikanda ili kuwezesha bidhaa na huduma za nchi kupenye kirahisi katika masoko ya kikanda na kimataifa.
Akizindua maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani,Mwaisumbe amesema kuwa kauli mbiu katika maadhimisho hayo yatumike kutafakari mchango wa viwango katika kuendeleza uchumi wa viwango hususani sekta ya madawa na vifaa tiba dhidi ya mapambano ya magonjwa ya mlipuko.
Aidha amesema baadhi ya bidhaa zimekuwa zikikwama mipakani kwasababu ya kukosa ubora unaotakiwa ambapo ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda kuzingatia viwango katika uzalishaji na biashara zao ili kujipatia uhakika wa masoko.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.David Cadinda amesema TBS kama mwanachama wa Shirika la viwango Afrika huadhimisha maadhimisho hayo kila mwaka kwa lengo la kuamsha uelewa wa umuhimu wa viwango kwenye sekta mbalimbali.
Kauli mbiu katika madhimisho yam waka huu ni “Umuhimu wa Viwango katika vifaa tiba na madawa katika kupambana na UVIKO 19 na magonjwa mengine ya kuambukiza ambayo yanaweza kujitokeza.”
Post A Comment: