Na,Jusline Marco;Arusha
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)wametoa semina kwa watoa huduma za Usafirishaji Mkoa wa Arusha juu ya matumizi ya tiketi mtandao ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika rasmi juni mosi mwaka huu.
Akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa huduma za uchukuzi, Wizara ya ujenzi na uchukuzi Aron Kisaka amesema lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kuhusiana na tiketi mtandao ambazo zimeanza kutumika April mosi mwaka huu kwa majaribio.
Aidha amesema tiketi mtandao itaondoa adha ya abiria kuuziwa tiketi kwa bei ya juu tofauti na ilivyopangwa na mamlaka husika na kutoa urahisi wa kukata tiketi kupitia cm ya mkononi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Udhibiti,Usafiri wa barabara LATRA Johancen Katano amesema semina hiyo ambayo imejumuisha wasafirishaji wa Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara ambapo taarifa za utumiaji wa mfumo huo zitatumika katika utozaji wa kodi na TRA.
Naye Afisa mfawidhi LATRA Mkoa wa Arusha katika semina hiyo amewataka wananchi kukubali teknolojia hiyo ili iwe rahisi katika utekelezaji wa huduma hiyo na kuwa wafuatiliaji wa vipindi mbalimbali vya radio na television vya kuelimisha umma kwa manufaa yao.
Post A Comment: