Na. Mwandishi wetu, Arusha


Viongozi wote wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha wanaufanya mradi wa ulinzi wa Mtoto kama agenda ya kudumu ili liweze kuleta tija katika Jamii.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe.Dadi Horace Kolimba alipokuwa akizindua mradi wa upanuzi wa ulinzi wa mtoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe John Mongella,katika uzinduzi  wa mradi huo Kimkoa.


Mradi wa ulinzi wa Mtoto umelenga kufika katika halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na kwakuanzia utaanzia Halmashauri 4 za Arusha Jiji, Arusha Vijijini Meru, na Karatu.


Amesema mradi huo utaweza kuwafikia watoto, vijana na familia na hii itasaidia kumaliza tatizo la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.


Aidha, ameyataka mashirika yasiyo ya Kiserikali kujitokeza na kubuni miradi itakayo tatua matatizo ya watoto wa mitaani.


Mwenyekiti wa bodi ya shirika la SOS  bwana Haruna Masebu amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha mtoto analelewa katika mazingira bora, yenye upendo na nidhani ili kujenga kizazi makini.


Aidha, imeiyomba serikali iendelee kushirikiana na SOS katika kutoa elimu ya sera ya mtoto katika Jamii.


Nae, Mkurugenzi Mtendaji kutoka SOS bwana David Mulongo amesema mradi huo utakuwa wa miaka 5 kuanzia 2022 hadi 2025 na umelenga kufikia makundi ya watoto ambao wataunganishwa na familia zao.


Pia, mradi utawafikia vijana wa mtaani kwa kuwajengea mazingira mazuri na pia familia zenye uchumi duni  nazo zitajengewe uwezo katika uchumi ili ziweze kujikimu mahitaji yake.


Amesema wanufaika wa moja kwa moja  wa mradi huo ni takribani watu  11,044  ambapo watoto watakuwa 2,220.


Mradi huo utatekelezwa kwa kufuata sera, taratibu na miongozo kutoka Serikalini ili kuufanya kuwa endelevu hata baada ya muda wa mradi kuisha.


Mratibu wa mpango wa  SOS kutoka TAMISEMI Bi. Mariam Hussein Nkumbwa Amesema jukumu la TAMISEMI ni kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora kwa wananchi kwa kushirikiana na Serikali za Mkoa na Halmashauri.


Mradi wa ulinzi wa Mtoto umezinduliwa rasmi kwa Mkoa wa Arusha na utatekelezaji ndani ya miaka 5 kuanzia 2022 hadi 2026 katika halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.

Share To:

Post A Comment: