Na mwandishi wetu.
Aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya awamu ya tano ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Mwanza Mheshimiwa Luaga Mpina ameingia kwenye mgogoro na wananchi wa Kijiji cha Dala Kata ya Mvuha Halmashauri ya Morogoro baada ya Kampuni yake ya MPSON’S CO LTD kudaiwa kumiliki eneo lenye ukubwa wa ekari mia saba (700 ) bila ya wananchi wa kijiji hicho kuridhia.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na Mpina inadaiwa kumilikishwa eneo hilo na kijiji cha Dala kinyume cha sheria kwa kuwa eneo lolote linalozidi hekali 50 kijiji hakina mamlaka ya kumilikisha bali kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 5 ni Kamishna wa ardhi ndio mwenye mamlaka ya hiyo.
Wakizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Kijiji waananchi wa kijiji hicho wamesema toka mwaka 2016 wamekuwa wakimlalamikia kiongozi huyo bila ya mafanikio yeyote licha ya kufika kwenye ngazi tofauti za serikali na chama cha mapinduzi CCM.
Kwa upande wake Idd Kibwana makazi wa kijiji cha Dala amesema mwaka 2018 mgogoro ulifika kwa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally na ambaye aliwapa matumaini kwa kuahidi kushughulikia suala hilo lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
“Tunakumbuka mwaka 2018 mwezi wa nane gazeti la mwananchi liliandika Dk Bashiru kupambana na Waziri anayemiliki ekari 1000, lakini licha ya kauli hiyo hatujaona lolote mpaka leo”. Alisema bwana Idd Kibwana .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Dala Mohamed Kilimasinde amesema mwaka 2016 Kijiji walishangaa kuona Mpina akimiliki ekari 700 kwa madai kuwa uongozi wa kipindi hicho ulimpatia bila ya kupitia mkutano mkuu wa kijiji ambao ndio wenye mamlaka ya kupitisha au kupinga maombi yeyote ya umiliki wa ardhi ya kijiji.
Aidha amesema mwaka 2017 uongozi wa Mkoa, Wilaya, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ilifika kijijini hapo ili kufahamu hitimisho la mgorogoro wa ekari 700 anazozimiliki Mpina ambapo ilionekana Serikali ya Kijiji ilifanya makosa kuidhinisha ekari zote hizo na haina mamlaka hayo na kwamba serikali kuu ndio yenye mamlaka.
“Kwa kauli yeke Mpina alisema kwa sababu eneo nimeshaanza kulima tangu mwaka 2009 basi hiyo milioni 35 iacheni ifanyakazi ya maendeleo.” Alisema mwenyekiti huyo.
Nae Diwani wa Kata ya Mvuha Mfaume Chanzi amewatoa hofu wananchi hao na kumuomba RAIS wa Jamuhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kusikiliza kilio cha wanannchi hao ambao wengine hawana hata mashamba ya kilima na kujipatia kipato cha kila siku.
Akizungumza kwa njia ya Simu Mhe Luaga Mpina amekiri kumiliki mashamba hayo licha ya kukiri amesema yupo tayari kukutana na wananchi hao kama watamuandikia barua ya wito na kutaka kukutana naye.
Post A Comment: