Changamoto zilizokuwa zikiwakabili wa wakulima wa mazao ya kimkakati ya Korosho na Mchikichi zinaelekea kuwa historia baada ya Camartec kuanza mchakato wa kutengeneza mashine za kubangulia mazao hayo sanjari na kuvunia hivyo kuongeza Mnyororo wa thamani.
Aidha upatikanaji wa mshine mpya za kisasa za Ubanguaji wa Korosho kutaongeza ubora na thamani na kuachana na njia ya kienyeji ya ubanguaji wa korosho unaosababisha korosho kuwa vipande vipande na kukosa ubora unaohitajika kwenye masoko ya kimataifa.
Hayo yamebainika wakati za ziara ya wanahabari watafiti na wabunifu waliokuwa katika mafunzo ya sayansi na teknolojia yaliondaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kituo cha zana za kilimo na teknolojia za vijijini CARMATEC Jijini Arusha.
Kituo hicho cha zana za kilimo na teknolojia vijijini kilichoanzishwa mwaka 1981 kwa sheria ya bunge namba 9 kilianza kazi rasmi mwaka mmoja baadae 1982 kufanya utafiti wa mashine za kilimo pamoja na majaribio pia uhaulishaji wa mashine za kilimo.
Aidha taasisi hiyo ya Camartec kwa kushirikiana na Temdo, Tirdo na Sido zilizo chini ya wizara ya viwanda na biashara zimekuwa zikishirikiana kwa pamoja kuhakikisha Adhma ya serikali ya awamu ya sita kufikia uchumi wa kati wa viwanda inafikiwa.
Kwa malengo hayo fuatana na makala haya kuweza kufahamu kwa kina jinsi serikali ya awamu ya sita kupitia kituo hicho kupita makala haya kujionea teknolojia za kilimo na teknolojia za vijijini zinazobuniwa na Camartec.
Ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za mashine mbalimbali za kilimo kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao hayo ya kimkakati kusaidia kuchakata mazao hayo hapa nchini hivyo kuongeza myororo wa thamani na kumpatia kipato mkulima.
Akiongea ofisini kwake mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa zana za kilimo ya Carmatec Mhandisi Pythias Ntella wakati akiohojiwa na mwandishi wa habari hizi anasema kuwa changamoto hizo zinaenda kuwa historia baada ya kuanza kutengeneza mashine za kubangulia Korosho na mashine za mchikichi za kuvunia na kubangua zao hilo.
Kwa mujibu wa Mhandisi Ntella anaeleza kuwa wanategemea baada ya kuja na mashine hizo kwa siku zijazo mkulima wa zao la korosho kuuza korosho iliyobanguliwa tayari hivyo kuongeza thamani ya mazao yake baada ya kutoka shambani tofauti na sasa kuuza korosho ghafi nje ya nchi.
Anasema kuwa wapo pia kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda darasa kwenye vijini cha kubangua korosho ambavyo vitatumika kubangulia korosho za wakulima ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kubangua korosho kwa wakulima jambo ambalo liyaongeza thamani ya mazao hayo na kumpatia mkulima faida badala ya kuuza korosho ghafi nje ya nchi.
“Ndugu wanahabari utafiti huu wa mashine kwa kuongeza thamani ya mazao utasaidia wakulima kujua kubangua kwa njia za kisasa na kutumia teknolojia ya kisasa na kuachana na teknolojia ya kienyeji ambayo imekuwa ikishusha thamani ya zao la korosho jambo hilo limepelekea walima kuuza korosha ghafi nje ya nchi na kuikosesha fedha ambazo kama tungeuza korosho mnyororo wa thamani ungeongezeka”
Mhandsi Ntella anaeleza kuwa Mchakato huu wa kutengeneza mashine hizi umetokana na adhma ya serikali ya awamu ya tano kuboresha na kuyapatia thamani mazao ya kimkakati ikiwemo mazao haya ya mchikichi na korosho kama kiwanda tukaona tufanye utafiti ndipo tukabaini changamoto zao na kuanza kuzifanyiakazi na kuja na majawabu haya ya kuanzisha viwanda darasa vya mazao hayo kwa kuyapa thamani na kuacha kuuza mazao ghafi nje ya nchi ili kuweza kulipanua soko la hapa nchini na nje ya nchi.
Anaeleza Kwamba utengenezaji wa viwanda darasa pia utaenda sambamba na mafunzo kwa wakulima kuweza kuanzisha viwanda vya kubangulia mazao hayo jambo ambalo litaleta mwamko mkubwa na hamasa ya uzalishaji wa mazao hayo na kusaidia kuongeza mnyororo wa tahamani badala ya sasa nchi kuuza mazao hayo nje .
“Bado kumekuwa na dhana ya wakulima wadogo kuona kuwa zana bora za kubangulia korosho na mchikichi nizakutoka nje ya nchi hili linatokana na kukosa uelewa hivyo elimu hiyo ya kiwanda darasa itawasaidia kupata mwamko wa kuanzisha viwanda vyao iwe kwa ushirika wa vikundi au mtu yeyote kuanzisha kiwanda ambacho wakulima wataleta mazao yao kuchakatwa”
Akielezea faida ya mashine hizo kwamba tofauti yake ni kuwa hizi mashine na njia za kienyeji ni kuwa mashine hizo zinatumika kuandaa mazao hayo kwa muda mfupi na ubora unaohitajika kwenye masoko ya kimataifa na hapa nchini na vipuri vyake vinapatikana humu humu nchini kwa bei rahisi kabisa.
Akiongelea zaidi mashine hizo anasema kwamba mashine hizo zinazotumia maganda ya korosho kuchemshia kama nishati jadididfu ni kitega uchumi kizuri kwa wakulima kuongeza mapato yao na mwisho wa siku tutaweza kuwasaidia kuweza kubangua mazao yao hapa nchini na kuondokana na uuzaji wa korosho ghafi nje ya nchi yetu na kulitosheleza soko la hapa nchini na ukanda wa Afrika mashariki.
Pia Mhandisi Ntella akaeleza kuwa wameendaa ramani ya ujenzi wa viwanda hivyo tena kwa ujenzi wa gharama nafuu ambazo zitawasaidia wakulima wadogo kuweza kumiliki viwanda hivyo kwa gharama ndogo kwani pia wametengeneza mashine za kufyatulia matofali ya udogo na saruji ambayo mkulima naweza kuimudu ghama hiyo.
Anasema kuwa mashine za mise za kutenganisha mbegu za michikichi sanajri na kuvunia zitasaida zao hilo kuondokana na kuzalisha kwa kiwango kidogo na kuongeza tija kwa kumuondolea mkulima adha ya upotevu wa mazao hivyo baada ya utafiti wetu tukagundua mkulima amekuwa akipoteza mazao mengi shambani ndio maana tumekuja na majawabu haya kuokoa mazao..
Amesema kuwa uwekezaji wa mashine unalingana na zao la kahawa hapa nchini kwani mkulima amekuwa akipeleka kahawa yake baada ya kuichakata na kubakia ganda la juu ambalo kiwanda ndio kimekuwa kikiweka thamani ya zao hilo kutoka awali mkulima kuanza kuchakata hivyo hata mazao hayo yakienda kwa utaratibu huo yataweza kuondokana na uuzaji wa mazao ghafi na kuacha kuwakatisha tamaaa wakulima.
Kwa muktadha huo akawataka wakulima kutokata tamaa ya kulima mazao hayo na badala yake kuanza kuchangamkia fursa ambayo ni mkakati wa serikali ya awamu ya tano kuongeza mnyororo wa thamani kwa kuweka mazao ya kimkakati ikiwemo mchikichi na korosho hivyo wao kuondoa dhana ya uuzaji wa mazao ghafi na kuja na mwarobaini wa kuanza kuchakata mzao hayo hapa nchini kabla hayajaenda sokoni.
“Tumelenga hata kwa mstaafu kuweza kuwa na kiwanda hata kama halimi mazao kwa kuanzisha kiwanda na kuwa kitenga uchumi baada ya kupata mafao yake kwani suala hili linawezekana kama vile wawekezaji wa mashine za kusaga mahindi wanavyofanya vile vile hata wao wanaweza kufanya hivyo kupitia uwekezaji wa aina hiyo hii itasaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na hivyo kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao hayo”
Awali mhandisi Godfrey Mwinama wa kituo cha kutengeneza zana za kilimo na teknolojia vijijini Carmatec akiongelea mashine hizo anasema kuwa ni kuitikia mwito wa serikali ya awamu ya tano ya kuwa na mazao ya kimkakati ambayo yatasaidia kuongeza kipato na kuwa na viwanda hapa nchini kuweza kuyachakata mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchini.
Anasema kuwa kabla ya Korosho kuuzwa nje ya nchi zitakuwa zimebanguliwa hapa nchini kupitia viwanda darasa ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kutoa elimu ya uanzishwaji wa viwanda hivyo kwa wakulima wadogo wa mazao hayo pia kuwaongezea thamani na vipato.
Anaeleza kuwa anaamini kuwa mtu mmoja mmoja anaweza kumiliki mashine hizo na mwisho wa siku asilimia kubwa ya wakulima kuweza kujifunza kubangua korosho na hivyo kuweza kupata masoko ya ndani na nchi jirani kwenye ukanda awa Afrika mashariki na Sadc badala kusubiria masoko ya Asia pekee..
Anabainisha kuwa uwepo wa mashine hizo hapa nchini utasaidia mazao hayo ya mchikichi na korosho kuongeza thamani yake na hivyo kuongeza wigo mpana wa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao hayo kwa kuongeza ulaji wa korosho na mafuta ya mawese ndani ya nchi na nje ya nchi.
Anasema kuwa mashine hizo zinaweza kuzalisha magunia nne ndani ya dakika 20 huku mtambo wa kufua mvuke kwa ajili ya kuziandaa krosho kubangulia una uwezo wa kuzalisha tani 3 hadi 4 kwa muda wa dakika 20 huku ikitumia maganda ya korosho yaliobanguliwa. Kama nishati jadidifu.
“Sasa utaona faida ya mashine hizi jinsi zitavyoweza kusaidia kuongeza tija ya mazao hayo na kuweza kuongeza mapato na thamani ya mazao kwa kuyachakata hapa nchini na kuondokana na kuuza mazao ghafi bila kuchakata nje ya nchi”anaeleza mhandisi Mwinama
Post A Comment: