Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida Anitha Msangi akiongoza mafunzo hayo.
Katibu wa Vijana wa chama hicho Mkoa wa Singida, Mary Gukwi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakishiriki michezo mbalimbali ya kuchangamsha viungo.
Michezo ikiendelea.
Michezo ikiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Na Dotto
Mwaibale, Singida
CHAMA cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kimetoa mafunzo kwa walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi katika Halmashauri za wilaya tatu mkoani Singida yaliyowalenga wasichanaa na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Mafunzo hayo yaliwahusisha walimu na wanajamii kutoka katika Halmashauri za wilaya yaIkungi, Singida DC na Manispaa.
Akizungumzia mafunzo hayo Afisa Mradi Msaidizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira kutoka TGGA, Praxeda Swai alisema mafunzo hayo ya siku nne yamewalenga walimu hao na wasichana ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na masuala ya tabia nchi na kugombea uongozi.
“Baada ya kuwapatia mafunzo haya walimu na wanajamii ambao tumewakutanisha hapa wataenda kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuchukua hatua chanya cha kukabiliana na changamoto za tabia nchi akitolea mfano Mkoa wa Singida ambao ulikuwa ukikabiliwa na ukame kutokana na ukataji wa miti” alisema Swai.
Alisema kazi kubwa watakayokuwa wakiifanya ni kuhamasisha jamii kupanda miti kwani wahanga wakubwa kunapokuwa na ukame ni wasichana na mama zao ambao wanakuwa wakiangaika kwenda kutafuta maji wakitumia muda mwingi na umbali mrefu na kuwa lengo lao ni kuifanya Singida kuwa ya kijani.
Mafunzo hayo yalioanza leo katika Ukumbi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida yatafunguliwa kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskas Muragili na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 10, 2022.
Post A Comment: