KITUO cha kuhamilisha teknolojia ya zana za kilimo Vijijini, Camartec,kimekuwa ni nguzo ya kutengeneza zana za kilimo na kuziuza kwa wakulima ndani na nje ya nchi ili kurahisisha shughuli za kimo.
Camartec,Imetoa teknolojia ya uzalishaji zana za kilimo na mashine mbalimbali kwa taasisi ya Imara tec,iliyowezesha kutengeza mashine mbalimbali na zana za kisasa ambazo zinatumika katika kilimo na kurahisisha uvunaji,kuongeza thamani ya mazao
Kutokana na kuwa ni kisima cha teknolojia Camartec,imeiwezesha kiufundi tasisi ya Imaratec,kubuni,kusanifu na kutengeneza mashine hizo za kisasa ambazo zinarahisisha shughuli za kilimo na kuongezaji thamani ya mazao
Kupitia uwezeshaji huo kutoka Camartec,taasisi ya Imara Tec,imeweza kubuni ,kusanifu na kutengeneza mashine na zana zingine za kilimo na kupata masoko makubwa ya kuuza zana hizo katika nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi
Hivyo Camartec,imejizatiti kuhakikisha inatoa teknolojia ya utengenezajiwa wa zana za kisasa za kilimo kwa taasisi yeyote yenye uhitaji ili itumike kuwanufaisha wawekezaji wazawa katika kutengeneza mashine , mitambo na zana zingine za kilimo na kuwawezesha wakulima kuboresha shughuli zao katika uzalishaji na uongezaji wa thamani ya mazao yao
Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya Imara tec,Alfred Chengura,anasema mafanikio hayo wameyapata kutokana na ufadhili uliotolewa na tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH, ambao umewezesha Camartec,kutoa teknolojia ya utengenezaji wa machine na zana za kilimo.
Imara tek,inajivunia ufadhili huo wa COSTECH,kwa kuwa umeaawezesha kupata teknolojia hiyo kutoka Camartec,na hivyo wamejipanga kuleta mapinduzi kwenye kilimo kwa kuzalisha zana za kutosha za kisasa kwa ajili ya kilimo.
Uwezeshaji huo umewezesha kutengenezwa mashine mbalimbali zenye ukubwa na uwezo tofauti kulingana na mahitaji ya mlengwa ambapo mashine hizo zina uwezo wa kupukuchua magunia 25 kwa saa moja na magunia 500 kwa siku
Anasema teknolojia hiyo inaiwezesha Imaratec , kuwa taasisi ya kwanza kunufaika na matumizi ya teknolojia kutoka Camartec,teknolojia ambayo imewezesha kubuni,kusanifu na kutengeneza mashine ili kurahisisha shughuli za kilimo
Anasema wepo wa COSTECH, umewezesha taasisi hiyo kuwa kimbilio la wakulima katika kupata za kisasa za kilimo na hivyo kutoa suluhisho kwa wakilima kuongeza uzalishaji wa mazao na mavuno
Post A Comment: