Moses Mashalla,Arusha
Benki ya Crdb nchini imesaini mkataba wa makubaliano wa mkopo na dhamana ya mikopo yenye jumla ya sh,182 bilioni kwa ajili ya kuiwezesha benki hiyo kukopesha wajasiriamali wa sekta mbalimbali nchini.
Katika mikopo hiyo benki ya Crdb itawakopesha wajasiriamali walio kwenye sekta ya kilimo,wajasiriamali wanawake ,pamoja na wajasiriamali ambao biashara zao ziliathirika na janga la UVIKO-19.
Akizungumza Leo katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Crdb Meru afisa Mkuu uendeshaji wa benki hiyo,Bruce Mwile alisema kwamba katika mikopo hiyo wateja wa benki hiyo pia watanufaika nayo kupitia tawi hilo.
"Hii ni fursa kubwa ambayo wateja pia watanufaika nayo kupitia tawi hili kwa kuwa benki yetu imesaini mkataba wa makubaliano wa mkopo wa dhamana ya mikopo yenye jumla ya sh,182 bilioni" alisema Mwile
Hatahivyo,alisisitiza kwamba pamoja na tawi la Crdb Meru kutoa huduma ya Premier Centre lakini vilevile imeboresha huduma kwa wateja kama utunzaji wa amana kupitia akaunti ya akiba,akaunti ya hundi kwa wafanyabiashara, akaunti ya malkia kwa wanawake pamoja na akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya watoto.
Mwili alisisitiza kwamba benki yao hivi karibuni tumepunguza riba kwenye mikopo binafsi kwa ajili ya wafanyakazi na wastaafu wa sekta ya umma kutoka asilimia 16 hadi 13 pamoja na mikopo ya kilimo kutoka asilimia 20 hadi 19.
Naye kaimu Mkurugenzi wa wa wateja wadogo na wa kati wa benki hiyo,Ericky Willy alisema kwamba alisema kuwa miongoni mwa huduma zinazopatikana kupitia tawi la Meru ni pamoja na huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kupitia mashine za ATM na kuwataka wateja kuchangamkia fursa hiyo.
Awali mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Mhandisi Richard Ruyango aliipongeza benki hiyo kwa kuwekeza kwenye mifumo ya kidijitali ya utoaji huduma kwa Simbanking, SimAccount,Internet Banking na Crdb Wakala.
"Benki ndicho chombo kikuu cha kutolea huduma za kifedha kwa wananchi hivyo benki zinatakiwa zizingatie mahitaji ya wananchi na ziweze kuwahamasisha kutambua umuhimu wa kutumia huduma za kibenki" alisema Ruyango
Post A Comment: