Na Angela Msimbira TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa , Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote nchini kusimamia vitendea kazi vilivyotolewa na Serikali ili viweze kutekeleza majukumu yaliyopangwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi
Akiongea leo tarehe 4 Aprili, 2022 kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugavi wa kilimo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Waziri Bashungwa amesema haitakuwa busara vitendea kazi vilivyotolewa kutumika kinyume na matarajio ya Serikali.
Waziri Bashungwa amesema ugawaji wa vifaa hivyo kutasaidia kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuwa ndio ilikuwa changamoto kwa maafisa ugani kwa muda mrefu hali iliyopelekea kutotimiza majukumu yao kwa weledi.
Amesema kuwa kwa muda mrefu serikali changamoto kubwa katika sekta ya kilimo hasa kwa maafisa ugani wa kilimo ni vitendea kazi hivyo kwa kugawa vitendea kazi kutasaidia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo
Amesema tayari Ofisi ya Rais –Tamisemi imeshakaa na wataalam wa Sekta ya kilimo kwa ajili ya kujadili muelekeo wa maboresho katika sekta hiyo,Hivyo ametoa wito kwa maafisa ugani wote nchini kufanyakazi kwa weledi kwa kuwa tayari serikali imewapatia vitendea kazi
Aidha, amevitaja vitendea kazi vilivyogawiwa kwa maafisa ugani kuwa ni pikipiki 6700, Vipima udongo (Soil Scanner) kwa Halmashauri 143 na vishikwambi kwa ajili ya kuingiza taarifa za kilimo.
Post A Comment: