Muungano wa AXIAN Telecom na Rostam Aziz leo umetangaza kukamilika kwa mchakato wa umiliki wa kampuni iliyounganishwa ya MIC
Tanzania Public Limited Company (Tigo na Zantel) katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Mchakato huu unaleta takribani wateja milioni 14 wa simu za mkononi kwa AXIAN Telecom na kuharakisha ukuaji wa
kampuni hii barani Afrika ambapo kwa sasa imefika nchi nane katika bara hili.
Kwa kununuliwa kwa MIC Tanzania PLC, AXIAN Telecom inafungua ukurasa
mpya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunayo furaha kuanza safari hii ya
kusisimua na wenzetu wa hapa (Tanzania) na ninaamini kwa pamoja tutafanikisha
mambo makubwa yatakayoendelea kuongoza mapinduzi ya kidijitali hapa nchini. Tunatoa shukrani zetu
kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kutusaidia kufanikisha mchakato huu, tunatarajia kuendelea kushirikiana
kwa pamoja.
Hassanein Hirdjee, Mwenyekiti wa AXIAN Telecom.
Muungano wa AXIAN Telecom umeweka vipaumbele vinne (4) muhimu katika kutekeleza majukumu yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
·
Kuendeleza mabadiliko ya kidijitali
nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na kutoa huduma zinazowanufaisha mtumiaji
mmoja mmoja na makampuni ya Kitanzania. Muungano huu una uwezo wa kutumia teknolojia za
mtandao wa kasi na nyaya za chini ya ardhi ambazo zitaleta mawasiliano ya haraka kati ya Watanzania na
kwingineko duniani.
·
Kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano
na kuongoza ujumuishwaji wa kidijitali kwa kuwekeza kikamilifu kwenye ujenzi wa
miondombinu ya mawasiliano. Muungano huu
unapanga kuimarisha upatikanaji na ubora wa mtandao hasa kupitia teknolojia ya 4G.
·
Kuongeza kasi ya ujumuishwaji wa huduma za kifedha
kwa njia ya simu za mkononi, kwa kuzingatia mafanikio ya huduma hizi kutoka
kwenye kampuni zilizounganishwa ili kuendeleza zaidi huduma za kifedha kwa njia
ya simu zinazolenga mahitaji ya wateja wa Tanzania. Umoja huo pia
utahakikisha muungano huu unafaidika kupitia utaalamu wake wa kutoa huduma za
kifedha za kiwango cha juu katika nchi zingine.
·
Kukuza na kuendeleza vipaji. Muungano huo
unakusudia kukuza maendeleo ya taaluma za wafanyakazi na kuweka mkazo mkubwa kwenye
mafunzo, kubadilishana uzoefu na kushirikishana maarifa ya pamoja miongoni mwa
wafanyakazi wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.
Muungano huu unajumuisha AXIAN Telecom na Bw. Rostam Azizi, mtanzania mfanyabiashara
na mjasiriamali ambaye ana taaluma ya muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano na amekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo
ya sekta hii hapa nchini Tanzania. Bw. Azizi, akiwa kama Mwenyekiti ajaye wa
MIC Tanzania PLC, atatoa mwongozo wa kimkakati na usimamizi wa kampuni na mfumo
mzima wa uendeshaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wadau wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.
Tulipoanza safari yetu ya mawasiliano
zaidi ya miaka ishirini iliyopita, suala kubwa lilikuwa kuunganisha watanzania
kwenye huduma hii. Tulikuwa waanzilishi katika kujenga mtandao wa huduma za simu, hasa katika maeneo
ya vijijini, ambapo kwa sasa Watanzania
wenzangu wengi wanafurahia huduma hii. Tukitazama malengo ya pamoja na AXIAN
Telecom, ni Dhahiri kuwa tutafanikiwa kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa
huduma za kidigitali nchini kote, tukizingatia
mahitaji muhimu kwa Watanzania na makampuni.
Rostam Azizi, Mwenyekitii MIC Tanzania PLC.
Ikitumia utaalamu wake hasa katika kusambaza
teknolojia za hali ya juu kama vile mitandao ya 5G na kuanzisha huduma za
kifedha kwa njia ya simu za mkononi zilizofanikiwa, AXIAN Telecom ina dhamira ya
kuupa nguvu mfumo wa mawasiliano hapa Tanzania hasa katika kuhakikisha kuwa
wateja wanapata huduma bora zaidi.
Post A Comment: