Wajumbe washauri wa baraza la Ardhi na nyumba wilayani humo kabla ya kuapishwa. Kutoka kushoto ni Charles Makala, Kitundu Kitundu, Hamisi Salim na Zulfa Mvungi.
Na Dotto Mwaibale, Mkalama
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imeingia katika historia baada ya kupata wajumbe watakaokuwa wakishauri na kusikiliza migogoro ya ardhi na nyumba huduma ambayo haikuwepo tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 2015.
Kupatikana kwa wajumbe hao na kuanza kusikiliza migogoro hiyo ya ardhi kutawapunguzia adha waliokuwa wakiipata wananchi wa wilaya hiyo ya kutembelea umbali mrefu kwenda kusikiliza mashauri yao wilayani Iramba hali iliyosababisha baadhi yao kupoteza haki zao kwa kukata tama ya kwenda kusikiliza kesi kutokana na umbali huo.
Akuzungumza leo baada ya kuapishwa kwa wajumbe hao ambao watakuwa washauri
wa baraza la ardhi na nyumba wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dk.Binilith Mahenge aliwataka waende kutenda haki wakati wa kutoa maamuzi yao
na kujiepusha na kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mahenge
aliwataka wajumbe hao kabla ya kuanza kazi hiyo iliyopo mbele yao jambo la
kwanza wanalopaswa kulifanya ni kwenda kuzisoma nyaraka zote zenye maamuzi ya mabaraza yaliyopita
ili waweze kuelewa upana na maamuzi mbalimbali yaliyofanyika katika mabaraza
hayo.
“
Nawashauri msianze kusikiliza kesi bila ya kujifunza kwa wiki mbili au zaidi
namna ya kuzisikiliza na kuzitatua na kujiongeza kusoma mambo mbalimbali
yanayohusu masuala ya utatuzi wa migogoro hiyo ” alisema Mahenge.
Dk.
Mahenge aliwataka wajumbe hao waende kutoa maamuzi bila ya kuiga yaliyowahi
kutolewa na mtu Fulani bali wajiridhishe baada ya kuyasikiliza na kutoa maamuzi
sahihi na si vinginevyo.
Aidha
Mahenge aliwaambia wajumbe hao kuwa wana kwenda kutatua kero ya migogoro ya
ardhi ambayo ni kubwa mno kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, kata hadi vijijini
hivyo jukumu lao ni kwenda kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuisaidia Serikali.
Mkuu
wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo alisema kwa muda mrefu wananchi walikuwa
wakipoteza haki kwa namna mbili ya kwanza kupindishwa na watoa maamuzi na mbili
ni kushindwa kumudu gharama za kwenda kusikiliza mashauri yao wilayani Iramba.
Aliwataka
wajumbe hao kwenda kufanya kazi kwa bidii na kuwatahadharisha kutolewa madaraka
kwani kumekuwa na tabia ya mtu akipata kazi miezi ya mwanzo anafanya vizuri
lakini baada ya muda mfupi hubadilika na kuonesha tabia yake isiyo nzuri hivyo
aliwata kuwa makini kwani wanapewa miezi sita ya matazamiao na kubaini kama
walichagua wajumbe wazuri au laa.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya hiyo James John Mkwega alisema kupatikana kwa baraza hilo
kwao ni tunu kubwa hivyo alitumia nafasi hiyo kuipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya na viongozi wote
walioshiriki kusaidia kupata baraza hilo.
“Tumepata
halmashauri hii tangu mwaka 2015 na tuliletewa huduma nyingi lakini huduma
iliyokuwa ikitutesa sana ni hii ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwani
wanamkalama wengi waliokuwa na kipato
kidogo walipoteza haki zao kwani walipokuwa wakikatiwa rufaa ya mashauri
yao kwenda Kiomboi walishindwa kutokana na umbali na gharama hivyo kupelekwa
kwa huduma hiyo makao makuu ya wilaya hiyo Nduguti kutatoa fursa kwa kila
mwananchi kupata haki yake” alisema Mkwega.
Mkwega aliwaambia wajumbe hao kuwa Wanamkalama zaidi ya 200,000 wamewapa dhamana ya kuwatumikia na kuwa hawahitaji baraza bali huduma hivyo wanaimani nao kubwa watamshauri mwenyekiti wao Baraka Shuma ili waweze kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuhakikisha haki inatendeka kwani kwa wanamkalama hakuna utajiri mkubwa kama ardhi hivyo ilkilindwa ardhi hiyo ambayo wamezoea kurithishana kwa utamaduni wao hata kwa Mwenyezi Mungu watabarikiwa.
Mwenyekiti
wa Baraza hilo, Baraka Shuma alishukuru kuanza kwa baraza wilayani humo na kuwa
kulikuwa na changamoto kubwa kwa wananchi ya kupata huduma kwa kutembea umbali
mrefu kuifuata Kiomboi Iramba hasa
kipindi cha mvua za masika.
Alisema
baraza hilo litaanza kufanya kazi wakati wowote baada ya idadi ya wajumbe
wasiopungua wawili kukamilika akiwepo Mwenyekiti na kula kiapo mbele ya mkuu wa
mkoa husika na kuwa jambo hilo ni la kihistoria katika wilaya hiyo.
Wajumbe hao washauri wa baraza la Ardhi na Nyumba walioapishwa ni Charles Makala, Kitundu Kitundu, Hamisi Salim na Zulfa Mvungi.
Post A Comment: