Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban akitazama eneo la upimaji wa mita za umeme mara baada ya kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani. Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani leo Machi 30, 2022. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban akikagua eneo la upimaji wa mita za maji mara baada ya kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani leo Machi 30, 2022. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban akizungumza jambo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa mara baada ya kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani.Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani leo Machi 30, 2022.Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban akimsikiliza Meneja Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani Bw. Alban Kihula mara baada ya kufanya ziara kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani leo Machi 30, 2022.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akipata picha ya pamoja na Mkurugenzi wa WMA, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ZAWEMA na Mkurugenzi wa ZAWEMA pamoja na watumishi wa WMA mara baada ya Waziri huyo kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani leo Machi 30, 2022.
********************
NA EMMANUEL MBATILO, PWANI
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban amefanya ziara ya kutembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani ili kujifunza namna gani wanaendesha kituo hicho katika kutoa huduma.
Akizungumza katika ziara hiyo Waziri huyo amesema kutokana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Wakala wa Vipimo Zanzibar (ZAWEMA) ambayo bado ni changa ipo fursa kubwa ya kujifunza kutoka kwa WMA ambao ni wazoefu wa muda mrefu.
"Tumeona mafanikio yao WMA, Serikali imeamua kwa makusudi kuiwezesha taasisi hii, taasisi hizi zinapowezeshwa bila shaka zinao watendaji wenye mawazo mazuri sna ya kufikia yale malengo ya kuanzishwa kwake". Amesema
Amesema wamejifunza namna wanavyohakiki maroli ya mafuta, mita za maji, mita za umeme na yote hayo inatumia teknolojia za kisasa na kuna ambayo zinatumia teknolojia za ndani zilizoibuliwa na wazalendo wa ndani.
Nae Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema ujio wa Wazii huyo ni muendelezo wa ushirikiano uliopo katika Jamuhiri ya Muungano wa Tanzania ambapo kimsingi taasisi hizi zinatakiwa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa amesema ziara hiyo ya waziri inaenda kuimarisha mahusiano yao ya awali ambayo wameshayaanza mwanzo na ZAWEMA.
Amesema ZAWEMA wanashirikiana nao kila wakati panapohitajika katika utekelezaji wa majukumu mfano wakati wanafanya ukaguzi wa vitendea kazi, ZAWEMA huleta vitendea kazi huku Bara kwaajili ya ukaguzi katika kuhakikisha kwamba vipimo vinavyopimwa Zanzibar na Tanzania bara zinafanana.
Mkurugenzi mtendaji wa Vipimo Zanzibar Bw. Mohammed Mwalim Simai amesema ziara yao imekuwa ya mafanikio kwasababu wamepata kile ambacho wamekitarajia kutoka kwa wenzao WMA katika kusimamia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba zile taasisi zinazofanya kazi zinazofanana baina ya Zanzibar na Tanzania Bara waweze kushirikiana.
Post A Comment: