Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo Machi 29 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori
Katika mazungumzo hayo Waziri Dkt.Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji kwa Wawekezaji wa kutoka Marekani hususani katika sekta ya Uwindaji wa Kitalii kwa kuzingatia maslahi ya nchi
" Moja ya shabaha yetu kama Wizara ni kuwavutia Wawekezaji, tunafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha Wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo wa Marekani wanawekeza katika uwekezaji huu wa muda mrefu'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kukusanya Sh23 bilioni kwa mwaka kutokana na uwekezaji mahiri unaoendekea kufanywa kwenye sekta ya utalii nchini
Post A Comment: