Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifungua mjadala kuhusu wanawake na vijana kumiliki ardhi uliofanyika tarehe 9 Machi 2022 jijini Dodoma. Sehemu ya washiriki wa mjadala kuhusu wanawake na vijana kumiliki ardhi uliofanyika tarehe 9 Machi 2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mjadala kuhusu wanawake na vijana kumiliki ardhi uliofanyika tarehe 9 Machi 2022 jijini Dodoma.

**********************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka jamii kuondokana na dhana potofu kuwa bado kuna mila na desturi kandamizi katika masuala ya umiliki wa ardhi kwa mwanawake.

Ameitaka jamii kujadili changamoto zinazowakabili wanawake na vijana juu ya umiliki wa ardhi sambamba na jamii kuhamasishwa kuachana na mila na desturi potofu kuhusu umiliki wa ardhi kwa makundi hayo.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula Fungu la 3 (2) la sheria namba 4 ya mwaka 1999 ni fungu mahsusi linalotambua haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki ,kutumia na kuuza au kugawa ardhi kwa viwango na masharti sawasawa na mawanaume.

Akizungumza wakati wa kufungua mjadala kuhusu wanawake na vijana kumiliki ardhi jijini Dodoma tarehe 9 Machi 2022, Waziri wa Ardhi alisema, sheria yoyote ya kimila itakayowanyima wanawake, watoto au watu wenye uleamavu uhalali wa kumiliki mali, kutumia ama kupata ardhi basi sheria hiyi ya mila itakuwa batili.

Alibainisha kuwa, Sheria za ardhi zimetoa kipaumbele kwa mwanamke kuwa na haki ya kumiliki ardhi isipokuwa mfumo wa kijamii, kisiasa na kiuchumi ndiyo unaomyima haki ya ardhi .

‘’Sababu za kijinsia kiutamaduni kijamii na kiuchumi ndizo zinazomyima haki mwanamke kwa kuwa hazitoi fursa rafiki kwa mwanamke’’ alisema Dkt Mabula.

Alitaka suala la elimu kupewa kipaumbele ili kuiwezesha jamii kuelewa haki za kisheria kwenye masuala ya umiliki wa ardhi na haki nyingine zinazohusu vijana na wanawake pamoja na watoto.

Aliviasa vyombo vya habari kutumia nafasi yake vizuri kwa kuwa jicho la serikali katika kutoa elimu na ufahamu kwa wananchi kuachana na mtazamo hasi kuhusu wanawake na kuunga mkono juhudi za serikali kumyanyua mwanamke na kijana kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Dkt Mabula aliitaka jamii kubadili fikra kuanzia katika ngazi ya familia kwa kuwa hatua hiyo itasaidia suala la mila na desturi kandamizi kuondoka kwa kuwa kizazi kitakuwa kimeona ubaya wa kile wazee waliokuwa wakikithamini.

Sambamba na hilo, aliwataka wazazi kuwa na tabia ya kutambua vipaji vya watoto wao wangali wadogo na kuhakikisha wanawaendeleza kupitia vipaji hivyo ili waweze kuwa wataalamu huko mbeleni katika masuala mbalimbali.

Naye Mwakilishi wa wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) Nuru Pipino alsema, wanawake na vijana wamekwa wakikabiliwa na changamo mbalimbali katika masuala ya ardhi ikiwemo kuota mizizi kwa mila na desturi potofu kwa wanawake na vijana pamoja na uelewa mdogo kwa mwanamke kumiliki ardhi.

‘’Kumekuwa na changamoto mbalimbali kuhusina na masuala ya ardhi kwa wanawake na vijana kama vile mila na desturi potofu sambamba na maeneo yanyochukuliwa na serikali kupewa kwa watu wenye fedha na kuachana makundi ya vijana na ardhi hiyo kukodishwa tena kwa makundi hayo’’ alisema Pipino.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: