Na Ahmed Mahmoud 
 
Wito umetolewa kwa Watanzania na wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kusaidia makundi yenye uhijitaji na hospitali za Pembezoni mwa miji ambazo zinakabiliwa na changamoto lukuki. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Nanenane Women Sacco's Happness Makundi wakati kikundi hicho kilipotembelea Hospital ya Wilaya ya Oltrument iliyopo Halmashauri Arusha DC wilayani Arumeru. 

 Amesema kwamba changamoto walizoziona zimewagusa na kuona kunasababu kwa wadau na serikali kuchukua hatua za haraka kupanua vyumba hivyo viendane na hadhi ya hospitali za Wilaya. Awali akitoa maelezo Matron wa hospital hiyo ya Wilaya Dorice Kahwa kwa wakinamama hao, amesema kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na ufinyu wa vyumba vya kuhifadhia Maiti Maabara chumba cha kufulia na ubovu wa jenereta hali inayofanya ukikatika umeme kuleta changamoto.


 "Ukiangalia kwa kina utaona hapa hatuna chumba cha Maiti hiki kilichopo hakina friji la kuhifadhia Maiti kwa Sasa kina uwezo wa kuhifadhi miili sita tu pia chumba cha Maabara ni finyu hakuna nafasi ya kupanga mashine"alisisitiza Kahwa 
 
Upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa hispital hiyo Lootosim Zablo amewashukuru wakinamama hao wa 88 Sacco's kwa msaada huo kwa hospitali hiyo kwani umekuja wakati muafaka Amesema kwamba pamoja na changamoto hizo nawaomba wadau wa maendeleo na watanzania wenzangu kuitupia macho ili kuisaidia hospital hiyo iendane na hadhi ya kiwilaya.

"Serikali  teyari walishakuja hapa na kupitia changamoto hizi najua ipo mbioni kzitatua ila kwa wale watakaoguswa tunawakaribisha kuja kusaidia ili wananchi wapate huduma za matibabu" 

Nae Meneja wa 88 Women Sacco's Leticia Cosmas msaada waliotoa unathamani ya milion 1.4 ikiwa ni pamoja na mashuka 40 ya wagonjwa,mashuka 5 chumba cha upasuaji Nguo za madaktari wa chumba cha upasuaji pamoja na Barakoa na kofia.

 Pia aliendelea kutaja vitu hivyo kuwa ni Maji Sabuni Dawa ya Meno Miswaki na Toilet Paper ambapo alibainisha kwamba huo ni taratibu wao wa kila Mwaka kurudisha kwa jamii ikiwa ni fungu la kumi la mapato yao.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment:

KARIBU WINNING SPIRIT PRE & PRIMARY SCHOOL ARUSHA

Winning Spirit Pre & Primary School Inawatangazia wazazi/Walezi wote wenye watoto waliofikia umri wa kuanza shule ya awali kuanzia miaka miwili na...

Jan 13 2025 - MsumbaNews Blog