Wafanyakazi wanawake wa Barrick wakifurahia Siku ya wanawake baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Katika kuelekea Siku ya wanawake Duniani 2022,Kampuni ya Barrick imeandaa semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wanawake katika migodi ya North Mara na Bulyanhulu.
Semina hizo zimejikita kuwawezesha kujua haki zao za msingi sambamba na kuwawezesha kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Barrick imeweka mkazo kwa kuongeza ajira za Wanawake katika sekta ya madini ambayo kwa jadi ilikuwa inatawaliwa na Wanaume kupitia mpango unaolenga kampeni ya ajira na mipango ya maendeleo kuwawezesha katika ngazi zote za kampuni.
Wafanyakazi wanawake wa Barrick na wadau wake pia waliweza kushiriki katika kongamano la wanawake mkoani Shinyanga, ambalo limeendana na uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, ambalo limekutanisha wanawake wa mkoa huo kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na upataji wa haki zao.
Kongamano hilo limefanyika wilayani Kahama, kwa kukutanisha wanawake wote wa Mkoa wa Shinyanga, limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8.
Wafanyakazi pia mbali na kujengewa uwezo walipata fursa ya kusherekea kwa kupata burudani kutoka kwa msanii mkongwe wa taarabu nchini Hadija Kopa.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea katika hafla ya Wanawake katika kuelekea kuadhimisha siku ya wanawake duniani
Wafanyakazi wakifurahia siku ya wanawake duniani
ASP Fatma Mtalimbo kutoka dawati la jinsia katika Jeshi la Polisi akiendesha semina kwa wafanyakazi wanawake wa Barrick katika mgodi wa North Mara kuelekea Siku ya Wanawake Duniani. Barrick imebadili mwelekeo wa kijinsia katika sekta ya madini
Mmoja wa wafanyakazi wa barrick Bulyanhulu akichangia mada wakati wa semina hiyo
Post A Comment: